Warumi 5 – Faida za Kuhesabiwa Haki kwa Imani
“Katika Biblia nzima hakuna sura nyingine inayoweza kufanana na haya maandishi ya ushindi.” (Martin Luther)
A. Faida za kuamini.
1. (1-2) Amani na kusimama kwa neema.
Basi tukiishahesabiwa haki kwa imani, tuko na amani kwa Mungu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye kwake tumepata njia ya imani kuifikia neema hii tunayosimama juu yake; na kufurahia katika tumaini la utukufu wa Mungu.
a. Kwa hivyo, baada ya kuhesabiwa haki kwa imani: Hadi hapa kwa Kitabu cha Warumi, Paulo ametushawishi sisi sote kuwa njia pekee ya wokovu ni kuhesabiwa haki kwa neema kwa njia ya imani. Sasa atatuambia manufaa halisi ya vitendo hili, akieleza kuwa ni zaidi ya wazo la kuvutia.
i. Kuhesabiwa haki kwa imani kunazungumza juu ya amri ya kisheria. Warumi 1:18–3:20 ilitupata na hatia mbele ya mahakama ya sheria ya Mungu, utukufu wa Mungu, na dhamiri yetu. Kisha Paulo akaeleza jinsi sababu ya kile Yesu alichofanya, haki ya Mungu inatolewa kwa wote wanaoamini. Hukumu ya hatia inageuzwa kuwa hukumu ya kuhesabiwa haki, na kuhesabiwa haki kwa imani.
b. Amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo: Hii ndiyo faida ya kwanza. Kwa sababu bei inalipwa kikamilifu na kazi ya Yesu msalabani, haki ya Mungu kwetu inatimizwa milele.
i. Hii si amani ya Mungu inayozungumzwa katika sehemu nyingine (kama vile Wafilipi 4:7). Hii ni amani na Mungu; vita kati ya Mungu na nafsi zetu imekamilika – naye alishinda, akatukomboa. Wengine hawakujua kamwe hawakuwa na amani na Mungu, lakini walikuwa kama madereva wanaopuuza taa nyekundu za gari la polisi kwenye kioo chao cha kutazama nyuma – wako katika shida hata kama hawajui, na hivi karibuni itawafikia.
ii. Amani hii inaweza tu kuja kupitia Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye na kazi yake ndiye msingi wetu wa amani. Kwa hakika, Yesu ndiye amani yetu (Waefeso 2:14).
iii. Kumbuka Biblia haisemi tuna amani na shetani, amani na ulimwengu, amani na mwili, au amani na dhambi. Maisha bado ni vita kwa Mkristo lakini si vita tena dhidi ya Mungu – ni kumpigania. Wakristo wengine wanajaribiwa kuamini kwamba vita dhidi ya Mungu vilikuwa mahali pazuri pa kuwa, na huo ni uwongo hatari na wa kulaaniwa.
iv. “Nimefurahi kupata dhambi inakuuma, na unaichukia. Kadiri chuki ya dhambi inavyozidi ndiyo bora. Nafsi inayochukia dhambi ni nafsi inayompenda Mungu. Ikiwa dhambi haikusumbui kamwe, basi Mungu hajawahi kukufadhili. (Charles Spurgeon)
c. Katika neema hii ambayo tunasimamia: Hii ni faida ya pili – tuna nafasi katika neema– katika neema ya Mungu isiyostahiliwa. Neema hii hutolewa kwa njia ya Yesu na kupatikana kwa imani.
i. Neema (neema ya Mungu isiyostahiliwa kwetu) si tu njia ya wokovu kuja kwetu, pia ni maelezo ya msimamo wetu wa sasa mbele za Mungu. Sio tu kanuni ya mwanzo wa maisha ya Kikristo, pia ni kanuni endelevu ya maisha ya Kikristo. “Tunasimama kutafsiri wakati uliyo kamili, unaotumiwa kwa maana ya sasa, na kwa wazo la mtazamo unaoendelea.” (Morris)
ii. Wakristo wengi huanza katika neema, lakini baadaye wanafikiri lazima waende kwenye ukamilifu na ukomavu kwa kushughulika na Mungu juu ya kanuni ya sheria – juu ya mawazo ya kulipwa na kustahili. Paulo alizungumza kinyume na jambo lili hili katika Wagalatia 3:2–3 na Wagalatia 5:1–4.
iii. Kusimama katika neema kunatuhakikishia: Mtazamo wa sasa wa Mungu kwa mwumini katika Kristo Yesu ni wa kibali, kuwaona katika hali ya furaha, uzuri, na raha. Sio tu eti anatupenda, bali Anatupenda kwa sababu tuko ndani ya Yesu.
iv. Kusimama katika neema kunamaanisha :
∙ Sio lazima nithibitishe kuwa ninastahili upendo wa Mungu.
∙ Mungu ni rafiki yangu.
∙ Mlango wa kuingia umefunguliwa kwake milele.
∙ Niko huru kutoka kwa “karatasi ya alama” – uwajibikaji umetatuliwa kwa Yesu.
∙ Ninatumia muda mwingi kumsifu Mungu na muda mchache wa kujichukia.
v. “Waasi wa zamani hawasamehewi tu kwa kuondolewa adhabu inayostahili; wanaletwa mahali pa upendeleo wa juu mbele za Mungu – neema hii ambayo ndani yake tunasimama. (Bruce)
vi. Mtazamo Sahihi wa Mwanadamu chini ya Neema. (William Newell)
d. Kupitia kwake pia sisi tuna njia kwa imani: Kuingia kwetu katika msimamo huu wa neema ni kwa imani tu, na kwa njia ya Yesu; hatuwezi kufanya kazi wenyewe katika msimamo huu. Kuingia sio tu katika msimamo wa neema, lakini katika nyua za mbinguni. Hii ni baraka zaidi ya amani na Mungu. Mtu anaweza kupatanishwa na mkuu wake, lakini asiletwe mbele yake.(Pooli)
i. Leon Morris juu ya ufikiaji: Wazo ni lile la kuanzishwa kwa chumba cha uwepo wa mfalme. Ufikiaji wa kupewa umepungukiwa, kwani unaacha bila kuonekana ukweli kwamba hatuji kwa nguvu zetu wenyewe, bali tunahitaji ‘mtangulizi’ – Kristo.”
ii. Wuest anamnukuu Thayer kuhusu ufikiaji: “Uhusiano huo wa kirafiki na Mungu ambapo tunakubalika Kwake na kuwa na uhakika kwamba Yeye ana mwelekeo mzuri kwetu.”
e. Tuna ufikiaji: Hali timilifu ya kitenzi cha kuwa na ufikiaji pia inaonyesha kuwa hii ni milki iliyo imara, kipawa cha milele. Kwa sababu msimamo wetu unategemea neema, tunaweza kusimama na kuwa na amani, kwa sababu tunajua ufikiaji wetu ni miliki ya milele. Haiwezi kuondolewa baadaye.
i. “Na ufikiaji huu kwa Mungu, au utangulizi wa uwepo wa Kiungu, unapaswa kuzingatiwa kuwa fursa ya kudumu. Hatuletwi kwa Mungu kwa ajili ya mahojiano, bali kubaki naye; kuwa nyumba yake; na kwa imani, kuutazama uso wake, na kutembea katika nuru ya uso wake.” (Clarke)
f. Furahini katika tumaini la utukufu wa Mungu: Hili ndilo hitimisho la kueleweka la amani kama hii na msimamo huo wa neema. Tunapohusiana na Mungu kwa kanuni ya matendo, furaha yoyote ni ya kimawazo na utukufu wowote unaofikiriwa huenda kwetu, sio Mungu.
i. Furahi ni neno ambalo kwa kawaida hutafsiriwa kama kujivunia. Inamaanisha “tumaini la ushindi, lenye ujasiri.” (Morris)
ii. Tumaini halikumaanisha kutokuwa na uhakika kwa Paulo. JB Philipps anatafsiri tumaini kama uhakika wa furaha.
g. Kuhesabiwa haki kwa imani: Tena, haya yote yanaleta maana baada ya kuhesabiwa haki kwa imani. Ikiwa hatuhesabiwi haki kwa neema kwa njia ya imani, basi hatuna amani na Mungu, na hatuna msimamo wa sasa wa neema.
i. “Ala, waumini wachache ndiyo walio na ujasiri wa imani! Wakati mtakatifu fulani hapa au pale anapoanza kuamini ukweli na kutembea katika uhuru wa kupiga kelele tunasema (labda kwa siri), ‘Lazima awe mtu mtakatifu hasa, aliyewekwa wakfu.’ Hapana, yeye ni maskini mwenye dhambi kama wewe, anayeamini katika wingi wa neema!” (Newell)
2. (3–4) Ahadi ya utukufu ni kwa wakati uliopo.
Wala si hivyo tu, ila sisi tunafurahi katika dhiki pia, tukijua ya kuwa dhiki huleta subira; na subira, tabia; na tabia, matumaini.
a. Na si hivyo tu, bali pia tunajivunia dhiki: Paulo anatazamia shtaka la kwamba yeye ni “andazi angani”, utukufu huo kwa Mkristo unahusu tu maisha ya baada ya kifo Paulo anajibu, “Najua tuna dhiki nyingi sasa, lakini twajivunia hizo pia.”
i. Paulo hazungumzii maneno ya kiroho. Kwanza, anatumia maneno makali. Dhiki ni “neno lenye nguvu. Halihusu usumbufu mdogo, lakini ugumu wa kweli” (Morris). Pili, Paulo aliishi maisha yaliyojaa dhiki. Paulo alijua ukweli wa jambo hili bora kuliko mtu mwingine yeyote.
b. Kujua kwamba dhiki huleta ustahimilivu: Tunaweza kujisifu katika dhiki (kihalisi, mikazo) kwa sababu ndiyo nafasi ya kuzaa subira (uvumilivu).
i. Mkimbiaji lazima akaziwe ili kupata uvumilivu. Mabaharia lazima waende baharini. Wanajeshi huenda vitani. Kwa Mkristo, dhiki ni sehemu tu ya maisha yetu ya Kikristo. Hatupaswi kutamani au kutumainia maisha ya Kikristo yasiyo na dhiki, hasa kwa sababu:
∙ Mungu anatumia dhiki kwa njia ya ajabu katika maisha yetu.
∙ Mungu anajua ni dhiki kiasi gani tunaweza kuchukua, na anapima kwa uangalifu dhiki tunayokabili.
∙ Wale ambao si Wakristo wanakabiliwa na dhiki pia.
ii. Mkristo anapaswa kuwa tayari kujaribiwa; awe radhi kuuiacha dini yake ijaribiwe. ‘Hapo,’ anasema, ‘torokea mbali kama unapenda.’ Je! unataka kubebwa mbinguni juu ya kitanda cha manyoya? (Spurgeon)
iii. “Nimesikia watu wakiwashauri wengine dhidi ya kuombea subira kwa sababu Mungu atawaletea dhiki. Kama hivyo ndivyo subira huja basi, ‘Mungu, leta shida.’ Nahitaji subira!” (Smith)
iv. “Fadhila zote ambazo dhiki inatupata ndani yake, inakua kikamilifu zaidi. Ikiwa mtu yeyote ni wa kimwili, dhaifu, kipofu, mwovu, mwenye hasira kali, mwenye majivuno, na kadhalika, dhiki itamfanya awe mtu wa kimwili zaidi, dhaifu, kipofu, mwovu na mwenye kukasirika zaidi. Kwa upande mwingine, ikiwa mtu ni wa kiroho, mwenye nguvu, mwenye hekima, mcha Mungu, mpole na mnyenyekevu, atakuwa kiroho zaidi, mwenye nguvu, mwenye hekima, mcha Mungu, mpole na mnyenyekevu zaidi.” (Martin Luther)
v. “’Dhiki huleta subira,’ asema mtume. Kwa kawaida si hivyo. Dhiki huleta kutokuwa na subira, na kutokuwa na subira hukosa matunda ya uzoefu, na huingia kwenye kukosa tumaini. Waulize wengi waliozika mtoto mpendwa, au wamepoteza mali zao, au wameteseka maumivu ya mwili, na watakuambia kuwa matokeo ya asili ya mateso ni kuzalisha chuki dhidi ya riziki, uasi dhidi ya Mungu, maswali, kutokuamini, kukosa amani, na kila aina ya uovu. Lakini ni badiliko la ajabu jinsi gani linalotokea wakati moyo unafanywa upya na Roho Mtakatifu!” (Spurgeon)
c. Uvumilivu, tabia; na sifa, tumaini: Huu ni mnyororo wa dhamani wa dhahabu wa ukuaji na ukomavu wa Kikristo. Fadhila moja hujengwa juu ya nyingine tunapokua katika kielelezo cha Yesu.
i. Mara nyingi kila Mkristo anataka kukuza tabia na kuwa na matumaini zaidi. Sifa hizi huchipuka kutokana na subira, ambayo huja kupitia dhiki. Tungetamani kuwa na tabia bora na tumaini zaidi bila kuanza na dhiki, lakini huo sio kielelezo na mpango wa Mungu.
ii. Ningetamani Mungu anyunyize uvumilivu na tabia na matumaini kwangu ninapolala. Ningeweza kuamka Mkristo bora zaidi! Lakini huo sio mpango wa Mungu kwangu wala kwa Mkristo yeyote.
iii. Kwa hiyo twasema- kwa kiasi, kwa unyenyekevu-tunasema juu ya dhiki, “Bwana, ilete. Najua unanipenda na unapima kwa uangalifu kila jaribu na una kusudi la upendo la kutimiza katika kila dhiki. Bwana, sitatafuta majaribu wala kutafuta dhiki, lakini sitazidharau au kupoteza tumaini zitakapokuja. Ninatumaini hakika upendo wako kwa kila jambo unaloruhusu.”
3. (5) Ushahidi wa tumaini: Upendo wa Mungu mioyoni mwetu sasa hivi, umethibitishwa na uwepo wa Roho Mtakatifu maishani mwetu.
Tumaini halivunji moyo, kwa maana upendo wa Mungu umekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na yeye aliye Mtakatifu. Roho tuliyopewa.
a. Sasa tumaini halikatishi tamaa: Tumaini ambalo dhiki hujenga ndani yetu si tumaini ambalo litakatisha tamaa. Tunahakikishiwa hili kwa sababu Mungu amethibitisha nia yake ya kukamilisha kazi yake ndani yetu – thibitisho ni upendo wa Mungu … uliomiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu ambaye tulipewa.
b. Upendo wa Mungu… uliomiminwa katika mioyo yetu: Kila Mkristo anapaswa kuwa na uzoefu huu, ili kuwa na ufahamu wa ndani wa upendo wa Mungu kwetu.
i. Hoja za kimantiki za Mtume Paulo katika Warumi ni za kushangaza lakini Kitabu cha Warumi hakikosi hisia au uzoefu wa uhusiano wa kibinafsi na Mungu. Paulo anataka tufikirie mawazo mema juu ya Mungu, lakini pia anataka tuwe na uzoefu ufaao na Mungu – upendo wa Mungu… uliomiminwa mioyoni mwetu.
ii. Upendo wa Mungu haujatolewa kwetu kwa hila, unamiminwa ndani ya mioyo yetu. Baadhi ya wakristo wanaishi kama ni mchepuko tu lakini Mungu anataka tujue kumiminwa kwa upendo Wake.
c. Roho Mtakatifu ambaye tulipewa: Hivi ndivyo upendo wa Mungu unavyowasilishwa – kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kutokuwa na ufahamu wa upendo wa Mungu mara nyingi kunaweza kuhesabiwa kuwa kukosa kujazwa na Roho Mtakatifu daima na kutembea katika Roho.
i. Upendo wa Mungu ni kama nuru kwa jicho pofu hadi Roho Mtakatifu afungue jicho hilo… na Roho Mtakatifu na awe ndani ya kila mmoja wetu, ili kumwaga upendo wa Mungu mioyoni mwetu. (Spurgeon)
ii. Kila aliye Mkristo ana Roho Mtakatifu (Warumi 8:9). Lakini si kila Mkristo anaishi katika utele wa Roho Mtakatifu (Waefeso 5:18), na si kila Mkristo anatembea katika Roho (Warumi 8:4–5).
4. (6–8) Ufafanuzi wa upendo wa Mungu kwetu sisi.
Tulipokuwa bado hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa maana ni nadra mtu kufa kwa ajili ya mwenye haki; labda mtu angethubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. Bali Mungu anadhihirisha upendo wake mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa wenye dhambi.
a. Tulipokuwa bado hatuna nguvu: Paulo anaeleza ukuu wa upendo wa Mungu. Ni upendo unaotolewa kwa wasiostahili, kwa wale wasio na nguvu, kwa waovu, kwa wenye dhambi. Hii inasisitiza ukweli sababu za upendo wa Mungu zinapatikana ndani Yake, si ndani yetu.
i. Watu hawa ni akina nani? Ni watu wagani wasiomcha Mungu na uwovu ambao Yesu aliwafia? Paulo alitumia sura mbili na nusu za kwanza za Kitabu cha Warumi akituambia kwamba sisi sote ni watu hao.
b. Kwa wakati ufaao Kristo alikufa kwa ajili ya wasiomcha Mungu: Mungu alimtuma Mwanawe kwa wakati mwafaka, kwa wakati ufaao. Huenda ilionekana kuchelewa kwa wengine lakini kazi ya Yesu ilifanyika kwa wakati mkamilifu katika mpango wa Mungu: utimilifu wa wakati ulipowadia, Mungu alimtuma Mwanawe (Wagalatia 4:4).
i. Ulimwengu uliandaliwa kiroho, kiuchumi, kilugha, kisiasa, kifalsafa na kijiografia kwa ajili ya kuja kwake Yesu na kueneza Injili.
ii. Kwa wakati ufaao pia ina maanisha Yesu alikufa kwa wakati uliosahihi kwa ajili yetu. Alikufa tulipokuwa wenye dhambi, tuliohitaji Mwokozi. Muda wake ulikuwa sahihi kabisa kwetu.
c. Kristo alikufa kwa ajili ya wasiomcha Mungu: Paulo alitaja wazo la dhabihu badala ya neno upatanisho katika Warumi 3:25. Hapa, analeta hoja tena kwa kusema Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Neno la kale laKigiriki ni neno huper, linalomaanisha “kwa ajili ya, kwa niaba ya, badala ya.”
i. Mahali pengine ambapo huper inatumika katika Agano Jipya hutusaidia kuelewa hili. Katika Yohana 11:50, tunasoma: wala hamwoni kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya [huper] watu. Wagalatia 3:13 inasema, Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu [huper].
ii. Kwa kusema kweli, Yesu alikufa kwa ajili yangu, lazima pia useme, Sina nguvu za kujiokoa. Mimi si mcha Mungu. mimi ni mwenye dhambi.” Yesu alikufa ili kuniokoa na kubadilisha haya.
iii. Utasema, ‘Lo, mimi ni mmoja wa watu wabaya zaidi duniani.’ Kristo alikufa kwa ajili ya wabaya zaidi duniani.’Oh, lakini sina uwezo wa kuwa bora.’ Kristo alikufa kwa ajili ya wale ambao walikuwa hawana nguvu, ‘Oh lakini kesi yangu inajihukumu yenyewe.’ Kristo alikufa kwa ajili ya wale waliohukumiwa kisheria. ‘Ay, lakini kesi yangu haina matumaini.’ Kristo alikufa kwa ajili ya wasio na tumaini. Yeye ndiye tumaini la wasio na matumaini. Yeye si Mwokozi wa wale waliopotea kwa sehemu, bali wa wale waliopotea kabisa.” (Spurgeon)
iv. “Ikiwa Kristo alikufa kwa ajili ya wasiomcha Mungu, ukweli huu hauwaachi wasiomcha Mungu kisingizio chochote ikiwa hawatakuja kwake na kumwamini hata kupata wokovu. La sivyo wangeliomba, ‘Hatufai kuja.’ Lakini ninyi ni waovu, na Kristo alikufa kwa ajili ya waovu, kwa nini isiwe kwa ajili yenu? (Spurgeon)
d. Kwa maana ni nadra sana mtu kufia mwadilifu: Upendo wa Mungu ni upendo unaopita hata upendo bora zaidi kati ya wanadamu. Mtu mwema anaweza kufa kifo cha kishahidi kwa ajili ya “sampuli” ya mtu mwema – kama vile mtu mwadilifu au mtu mwema. Lakini Yesu alikufa kwa ajili ya wale ambao hawakuwa wenye haki wala wema.
i. Je, kuna tofauti kati ya mtu mwenye haki na mtu mwema katika mawazo ya Paulo? Tofauti katika Warumi 5:7 inaonekana kuwa mtu mwenye haki ni huyo tu – mwenye haki katika maisha yake ya kibinafsi lakini labda kukosa hisia kwa wengine. Mtu mwema kwa kulinganisha huenda zaidi ya mtu mwingine k pia kuwa mkarimu na mfadhili.
e. Lakini Mungu anaonyesha upendo wake mwenyewe: Je, kifo cha Mwana kinaonyeshaje upendo wa Baba? Kwa sababu ilikuwa vigumu zaidi kwa Baba kumtuma Mwanawe pekee, na ni kwa sababu Mungu [Baba] alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake (2 Wakorintho 5:19).
i. “Ingekuwa rahisi kuuona msalaba kuwa unaonyesha kutojali kwa Mungu, Mungu ambaye aliruhusu Yesu asiye na hatia kuchukuliwa na watu waovu, kuteswa, na kusulubiwa wakati hakufanya chochote… Isipokuwa Baba na Kristo ni moja, sio upendo wa Mungu ambao msalaba unaonyesha. (Morris)
ii. Kazi ya Yesu msalabani kwa ajili yetu ni thibitisho kuu la Mungu la upendo wake kwako. Anaweza kutoa ushahidi wa ziada, lakini hawezi kutoa uthibitisho mkubwa zaidi. Ikiwa msalaba ni onyesho kuu la upendo wa Mungu kwetu,basi pia ni onyesho kuu la chuki ya mwanadamu. Pia inathibitisha kwamba kimo cha chuki ya mwanadamu hauwezi kushinda kimo cha upendo wa Mungu.
iii. Udhihirisho wa upendo wa Mungu hauonyeshwi sana kwa kuwa Yesu alikufa, lakini unaonekana ndani yake ambaye Yesu alimfia – wenye dhambi wasiostahili na waasi dhidi yake.
5. (9–11) Wokovu wa kuepuka ghadhabu ya Mungu.
Tukihesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kupitia kwake. Kama tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa kifo cha Mwanawe, zaidi baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, bali pia tunafurahi katika Mungu kwa Bwana yetu Yesu Kristo, ambaye kwake sasa tumeupokea upatanisho.
a. Basi zaidi sana, tukiisha kuhesabiwa haki kwa damu yake, tutaokolewa na ghadhabu: Ikiwa tunahesabiwa haki kwa kazi ya Yesu, tunaweza kuwa na uhakika sisi pia tumeokolewa na ghadhabu kwa njia yake. Ghadhabu ya Mungu iliyodhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu (Warumi 1:18) iliwekwa juu ya Yesu badala ya mwumini.
i. Kwa asili, wengine wana mwelekeo wa kutanguliza ahadi hizo kuu za Mungu kwa “vidogo zaidi basi” kujihusu. Mungu anataka waone wazi: na Zaidi sana ni upendo na wema wa Mungu tuliopewa na zaidi tunaweza kuwa na imani naye.
ii. Kuokolewa kutoka kwa ghadhabu: Ghadhabu ya nani? hasira ya haki ya Mungu. Ni kweli yatupasa kuokolewa kutoka kwa ulimwengu, mwili, na shetani lakini zaidi ya yote tunapaswa kuokolewa kutokana na ghadhabu ya haki ya Mungu.
iii. John Trapp juu ya mengi zaidi: “Ni kazi kubwa zaidi ya Mungu kuwaleta watu kwenye neema, kuliko kuwa katika hali ya neema, kuwaleta kwenye utukufu; kwa sababu dhambi ni mbali na neema kuliko neema ilivyo mbali na utukufu.”
b. Tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu: Ikiwa Mungu alionyesha upendo huo wa ajabu kwetu tulipokuwa adui, fikiria baraka ambazo tutafurahia mara tu tutakapopatanishwa na Mungu! Ikiwa Mungu anafanya hili kwa ajili ya adui zake, ni zaidi gani atawafanyia marafiki zake!
i. Wuest, akimnukuu Alford: “Sio kwamba mtu aliyepatanishwa ana ujasiri ya kuepuka ghadhabu ya Mungu, lakini ujasiri wa ushindi pia – tumaini la furaha katika Mungu.”
c. Mengi Zaidi, baada ya kupatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake: Upatanisho huu hausaidii tu tunapokufa; pia inagusa maisha yetu ya sasa. Mungu milele anashughulika na waumini kwa msingi wa ghadhabu. Anaweza kuwaadhibu kama Baba mwenye upendo, lakini si kwa adhabu au malipo ya dhambi zao. Mungu huruhusu tu kuadhibu kuleta marekebisho ya upendo na mwongozo.
∙ Kuamini, na kukubali kupendwa wakati hatufai, ndiyo siri kuu.
∙ Kukataa kufanya maazimio na nadhiri; kwa maana huko ndiko kuutumainia mwili.
∙ Kutarajia kubarikiwa, ijapokuwa tukitambua zaidi na zaidi ukosefu wa thamani.
∙ Kushuhudia wema wa Mungu, nyakati zote.
∙ Kuwa na hakika ya upendeleo wa Mungu ujao; lakini kuwa na dhamiri ya upole zaidi kwake.
∙ Kutegemea mkono wa kuadibisha wa Mungu kama alama ya wema wake.
∙ Mtu aliye chini ya neema, kama Paulo, hana mizigo wa nafsi yake; lakini ana mizigo nyingi kuhusu wengine.
d. Kuokolewa, kuepuka ghadhabu kupitia yeye … tulipatanishwa na Mungu kwa kifo cha Mwanawe … furahini katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo … ambaye kwake sasa tumepokea upatanisho: Jambo hilo linasisitizwa.Cha muhimu ni kile tunacho kupitia Yesu. Kile tulicho nacho kupitia kazi zetu wenyewe hakijalishi na hakiwezi kutusaidia. Yote ni kupitia Yesu.
B. Wanaume Wawili.
1. (12) Kuenea kwa dhambi katika kizazi cha wanadamu.
Kwa hivyo, kama vile dhambi iliingia ulimwenguni kwa mtu mmoja, na kifo kupitia dhambi; kwa hivyo mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi;
a. Kama vile kupitia mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni: Mtume Paulo aliona Mwanzo 3 kuwa kweli kabisa, kihistoria. Kulingana na Paulo (na kulingana na Yesu, katika Mathayo 19:4–6), Adamu na Hawa walikuwa watu halisi na walichofanya kina matokeo ya kudumu hadi siku ya leo.
i. Ni muhimu kuelewa akaunti ya Adamu na Hawa si kifungu cha hiari cha kukubaliwa au kukataliwa, au kufananishwa. Kulingana na mada ya Paulo katika Warumi 5, huwezi kuondoa ukweli wa Mwanzo 3 bila kuondoa kanuni zinazoweka msingi wa wokovu wetu.
ii. “Kulingana na Paulo, Adamu alikuwa zaidi ya mtu wa kihistoria, mtu wa kwanza; pia alikuwa kama jina lake linamaanisha katika Kiebrania – ‘ubinadamu.’ Ubinadamu wote unatazamwa kuwa ulikuwepo hapo mwanzo katika Adamu.” (Bruce)
b. Kupitia mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni: Paulo hathibitishi hili, anaikubali tu kama ukweli kutoka Mwanzo 3 – dhambi iliingia ulimwenguni kupitia Adamu. Jambo la maana ni Adamu ndiye anayehusika na kuanguka kwa mwanadamu, si Hawa. Hawa alidanganywa alipofanya dhambi lakini Adamu alitenda dhambi akiwa na ufahamu kamili (1Timotheo 2:14).
c. Na kifo kupitia dhambi: Kifo kiliingia ulimwenguni na kuenea kwa watu wote kwa sababu ya dhambi ya Adamu. Mungu alimuahidi Adamu, siku utakapokula matunda yake hakika utakufa (Mwanzo 2:17). Kanuni ya kifo ilianzishwa ulimwenguni wakati Adamu alifanya dhambi na imetawala duniani tangu wakati huo. Kila kaburi ni ushahidi wa kuenea na kutawala kwa dhambi tangu wakati wa Adamu.
d. Hivyo kifo kikaenea kwa watu wote, kwa sababu wote walifanya dhambi: Kifo na dhambi vinauhusiano, watu wote ni wenye dhambi – kwa sababu wote wako chini ya kifo. Mtu asiye na dhambi hayuko chini ya kifo, lakini kwa kuwa kila mtu yuko chini ya kifo – hata mtoto mchanga – nithibitisho wote [wanadamu] walitenda dhambi katika Adamu.
i. Hii inaonekana isiyo ya kawaida kwa masikio yetu ya kibinafsi, lakini Paulo anafundisha wazi kwamba sisi sote tulitenda dhambi “katika” Adamu. Adamu ndiye baba wa kila mtu duniani; kila mwanadamu ambaye amewahi kuishi alikuwa “katika” chembe za urithi za Adamu. Kwa hiyo, wanadamu wote walitenda dhambi ndani ya Adamu.
ii. “Wote walitenda dhambi katika kisa hiki maana yake ni ‘wote walifanya dhambi katika Adamu’; Dhambi ya Adamu ni dhambi ya wote.” (Morris)
iii. Wanadamu ni wa kufa – chini ya kifo – kabla ya kutenda dhambi yoyote. Kwa kuwa mauti ni matokeo ya dhambi, inaonyesha kwamba sisi tumefanywa kuwa wenye dhambi kwa dhambi ya Adamu, si kwa dhambi zetu wenyewe.
iv. Huenda tusipendezwe na ukweli yakuwa tunafanywa wenye dhambi kwa kazi ya mtu mwingine. Tunaweza kupinga, na kusema, “Nataka kusimama kwa miguu yangu, nisifanywe mwenye dhambi kwa sababu ya kazi ya mtu mwingine.” Hata hivyo, ni haki kufanywa wenye haki kwa kazi ya mtu mwingine ikiwa tunafanywa wadhambi kwa kazi ya mtu mwingine. Ikiwa hatujafanywa kuwa wenye dhambi na Adamu, basi ni haki kufanywa wenye haki na Yesu.
e. Watu wote: Ukweli huu unaweza kutukosesha raha, lakini bado ni ukweli. Mtoto mdogo ni mwenye dhambi, anayekabiliwa na kifo. Daudi alielewa hili alipoandika, mimi nilizaliwa katika dhambi mama yangu alinichukua mimba hatiani (Zaburi 51:5).
i. Tunaweza pia kujua tumezaliwa tukiwa wenye dhambi kwa sababu nyinginezo. Kwanza, fikiria jinsi mtoto mdogo anawezakuwa mbinafsi na mwenye hasira. Pili, fikiria jinsi ambavyo hatuhitaji kamwe kuwafundisha watoto wetu kuwa wabaya – wanajifunza hilo peke yao, huku Adamu mzee akifundisha masomo.
ii. Ikiwa watoto wachanga ni wenye dhambi, inamaanisha wanaenda motoni? Si lazima. Kwanza, tunajua watoto wa waamini wanatakaswa kwa uwepo wa mzazi anayeamini (1 Wakorintho 7:14). Pili, Daudi alikuwa na uwumini kwamba mtoto wake angekutana naye mbinguni (2 Samweli 12:23). Hatimaye, tunajua mwisho wa yote, Mungu, ni mwamuzi wa ulimwengu wote, atafanya haki (Mwanzo 18:25).
iii. Ikiwa kuna watoto wa wazazi wasioamini mbinguni, ni muhimu kuelewa sio kwamba hawana hatia. Kama wana na binti za Adamu wenye hatia, kila mmoja wetu amezaliwa na hatia pia. Ikiwa watoto kama hao wataenda mbinguni, si kwa sababu hawana hatia wanaostahili mbinguni, bali ni kwa sababu ya rehema nyingi za Mungu zimeongezwa kwao pia.
2. (13-14) Pingamizi likajibu: “Nalidhani sisi tu wenye dhambi kwa sababu tuliivunja sheria.”
(Tangu wakati wa sheria dhambi ilikuwako ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi wakati hakuna sheria. Hata hivyo kifo kilitawala kutoka Adamu hadi kwa Musa, hata juu ya wale ambao hawakufanya dhambi kwa mfano wa kosa la Adamu, ambaye ni mfano wake ukia ajaye.
a. Hata mpaka wakati wa sheria dhambi ilikuwako ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwiwakati hakuna sheria: Tunajua chanzo cha yote tunafanywa kuwa wenye dhambi kwa sababu ya Adamu na si kwa sababu sisi wenyewe tunavunja sheria.
i. Sheria ilichelewa sana kuzuia dhambi na mauti na ni dhaifu sana kuweza kuokoa kutoka katika dhambi na mauti.
b. Hata hivyo mauti alitawala: Utawala wa mauti usio na huruma – hata kabla ya sheria kutolewa wakati wa Musa – inathibitisha kwamba mwanadamu alikuwa chini ya dhambi kabla ya sheria. Mauti ilitawala… hata juu ya wale ambao hawakuwa wametenda dhambi sawasawa na Adamu, ikionyesha kwamba kanuni ya dhambi ilikuwa ikifanya kazi ndani ya kila mwanadamu.
c. Adamu, ambaye ni mfano wa Yeye ambaye angekuja: Paulo anawasilisha Adamu kama mfano– picha, uwakilishi – wa Yesu. Wote wawili Adamu na Yesu walikuwa watu wasio na dhambi kabisa tangu mwanzo, na wote wawili walifanya mambo ambayo yalikuwa na matokeo kwa wanadamu wote.
3. (15–17) Tofauti kati ya kazi ya Adamu na kazi ya Yesu.
Lakini zawadi ya bure si kama kosa. Ikiwa kwa kosa la mtu mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na zawadi kwa neema ya mtu mmoja, Yesu Kristo, ilizidi kwa wengi. Na zawadi si kama ile iliyotolewa na yule aliyetenda dhambi. Kwa maana hukumu iliyotokana na kosa la mmoja na ilileta hukumu, lakini zawadi ya bure iliyotokana na makosa mengi ilileta kuhesabiwa haki. Kwa maana ikiwa kwa kosa la mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya huyo mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa huyo Mmoja, Yesu Kristo.)
a. Lakini zawadi ya bure si kama kosa: Adamu alitoa kosa lililokuwa na matokeo kwa wanadamu wote – kwa sababu ya kosa la Adamu, wengi walikufa. Yesu anatoa zawadi ya bure ambayo ina matokeo kwa jamii nzima ya wanadamu, lakini kwa njia tofauti. Kwa kipawachabure cha Yesu, neema ya Mungu… ilizidi kwa wengi. Kazi ya Adamu ilileta mauti lakini kazi ya Yesu inaleta neema.
b. Wengi walikufa: Hii inaanza kuelezea matokeo ya kosa la Adamu. Zaidi ilikuja: hukumu, iliyosababisha hukumu, na kifo kilitawala juu ya wanadamu. Lakini pia kuna matokeo ya zawadi ya bure ya Yesu: neema ilizidi kwa wengi, kuhesabiwa haki (kwa sababu makosa mengi yaliwekwa juu ya Yesu), neema nyingi, zawadi ya haki, na kutawala katika maisha.
i. “Hasemi kwamba kifo kilitawala sisi sote kwa sababu sote tulifanya dhambi; anasema kwamba kifo kilitawala sisi sote kwa sababu Adamu alifanya dhambi.” (Morris)
c. Kifo kilitawala… haki itatawala: Tunaweza kusema kwamba wote wawili Adamu na Yesu ni wafalme, kila mmoja akianzisha utawala. Chini ya Adamu, kifo kilitawala. Chini ya Yesu, tunaweza kutawala maishani kupitia yule Mmoja, Yesu Kristo.
i. Inashangaza kufikiria jinsi kikamilifu kifo kimetawala chini ya Adamu. Kila mtu aliyezaliwa hufa – kiwango cha vifo ni 100%. Hakuna anayesalia. Mtoto anapozaliwa, si suala la iwapo mtoto ataishi au atakufa – hakika atakufa; swali pekee ni lini. Tunaufikiria ulimwengu huu kama nchi ya walio hai, lakini kwa kweli ni nchi ya wanaokufa, na mabilioni ya miili ya wanadamu iliyotupwa duniani kwa karne nyingi inathibitisha hilo. Lakini Paulo anasema utawala wa uzima kupitia Yesu ni hakika zaidi. Utawala wa mwamini katikamaisha kupitia Yesu ni hakika zaidi kuliko kifo au kodi!
4. (18) Mukhtasari: watu wawili.
Basi, kama kwa kosa la mtu mmoja hukumu ilikuja kwa watu wote, hata hukumu ikaleta hukumu; vivyo hivyo kwa tendo la haki la mtu mmoja kipawa cha bure kiliwajia watu wote, hata kuhesabiwa haki kwa uzima.
a. Kosa la mtu mmoja… Tendo la haki la Mtu mmoja: Kutokana na kifungu hiki, Adamu na Yesu wakati mwingine wanajulikana kama watu wawili. Kati yao wanawakilisha ubinadamu wote, na kila mtu anatambulishwa kama Adamu au Yesu. Tunazaliwa kutambuliwa na Adamu; tunaweza kuzaliwa mara ya pili katika utambulisho na Yesu.
i. Wazo la Adamu na Yesu kama wawakilishi wa jamii ya wanadamu wakati mwingine huitwa Theolojia ya Shirikisho, au Adamu na Yesu hujulikana kama Wakuu wa Shirikisho. Hii ni kwa sababu chini ya mfumo wa serikali ya shirikisho, wawakilishi huchaguliwa, mwakilishi huzungumza kwa niaba ya waliomchagua. Adamu anazungumza kwa ajili ya wale anaowawakilisha, na Yesu anazungumza kwa ajili ya watu wake.
ii. Tena, mtu anaweza kupinga: “Lakini sikuwahi kuchagua Adamu aniwakilishe.” Bila shaka ulifanya! Ulijitambulisha na Adamu kwa dhambi ya kwanza uliyo kufanya. Ni kweli kabisa tulizaliwa katika utambulisho wetu na Adamu, lakini pia tunauchagua kwa matendo yetu binafsi ya dhambi.
b. Kutokeza hukumu… na kusababisha kuhesabiwa haki: Matokeo ya uchaguzi huu – kumchagua Adamu au Yesu – inamaanisha kila kitu. Tukimchagua Adamu, tunapokea hukumu na ghadhabu. Tukimchagua Yesu, tunapokea zawadi yabure ya neema ya Mungu na kuhesabiwa haki.
c. Zawadi ya bure ilikuja kwa watu wote: Je, hii ina maanisha watu wote wanahesabiwa haki kwa zawadi ya bure? Bila kufanya uchaguzi wa kibinafsi, kila mtu alipokea laana ya kosa la Adamu. Je, ni kweli kila mtu, mbali na chaguo lake la kibinafsi, atapokea manufaa ya utiifu wa Yesu? Hapana. Kwanza, Paulo anaweka wazi zawadi ya bure si kama kosa – hazifanani katika matokeo yao au katika matumizi yao. Pili, zaidi ya mistari mitatu Paulo anaita kazi ya Yesu kuwa zawadi ya bure, na yeye kamwe hatumii maneno hayo kuhusisha kazi ya Adamu. Ni asili tu ya zawadi ambayo ni lazima ipokelewe kwa imani. Hatimaye, Paulo anafundisha waziwazi kote katika Agano Jipya kwamba wote hawajaokolewa.
i. Ni katika maana gani zawadi ya bure ilikuja kwa watu wote? Ilikuja kwa maana zawadi inatolewa, lakini si lazima ipokelewe.
ii. Wazo la watu wote wanaokolewa na kazi ya Yesu iwe wanajua au hawalijui inajulikana kama mafundisho wazi ya ulimwengu mzima. “Ikiwa fundisho la wazi la ulimwengu kote linafundishwa hapa, Paulo angekuwa anajipinga mwenyewe, kwa sababu tayari amewaonyesha watu wanaoangamia kwa sababu ya dhambi.” (Harrison)
5. (19) Muhtasari kinyume.
Kama kuasi kwa mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, hivyo basi kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki.
a. Kwa kutotii kwa mtu mmoja: Kutotii kwa Adamu kunafanya wanadamu kuwa watenda dhambi. Utiifu wa Yesu huwafanya wengi kuwa waadilifu. Kila mwakilishi huwasilisha matokeo ya kazi yao kwa “wafuasi” wao.
b. Wengi walifanywa wenye dhambi: Paulo anasisitiza jambo hilo tena. Katika mizizi, tulifanywa kuwa wenye dhambi kwa kazi ya Adamu. Bila shaka, tulimchagua Adamu wakati sisi binafsi tulitenda dhambi. Lakini kanuni inabakia kuwa mtu mwingine alitufanya wenye dhambi, tunaweza kufanywa wenye haki kwa kazi ya mtu mwingine.
i. Hii ndiyo njia pekee ya kazi ya Yesu kutufaidi kwa njia yoyote ile. Ikiwa kila mtu lazima ajitegemee, bila uwakilishi wa Adamu au Yesu, basi sote tutaangamia. Hakuna ambaye angeokolewa, kwa sababu kila mmoja wetu anatenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Ni mtu asiye na dhambi kwa niaba yetu ndiye anayeweza kutuokoa, na ni haki kwake kuchukua hatua kwa niaba yetu kwa sababu mtu mwingine alituweka katika uchafu huu kwa niaba yetu.
ii. Ikiwa niliiba benki na kupatikana na hatia ya uhalifu huo, rafiki yangu hataweza kumwambia hakimu, “Mheshimiwa, ninampenda rafiki yangu na ninataka kutumikia kifungo chake. Nitasimama mahali pake na kupokea adhabu anayostahili.” Hakimu angejibu, “Upuuzi. Hatutakuadhibu kwa uhalifu wake. Haitakuwa sawa. Alifanya uhalifu, kwa hivyo lazima apate adhabu. Ingekuwa haki kwa mtu mwingine kulipa adhabu ikiwa ningekuwa na hatia kwa sababu ya kazi ya mtu mwingine.
iii. Mtu anayesema, “Sitaki kuwakilishwa na Adamu au Yesu; Nataka kujiwakilisha” haelewi mambo mawili. Kwanza, haelewi si juu yetu. Hatukutunga sheria, Mungu alifanya. Pili, haelewi haki yetu binafsi mbele za Mungu ni kama nguo chafu (Isaya 64:6). Kwa Mungu, haki yetu ya kibinafsi ni bandia yenye kuudhi; kwa hivyo kusimama mwenyewe kunahakikisha kuangamizwa.
6. (20a) Kusudi la Sheria.
Zaidi ya hayo sheria iliingia ili kosa liongezeke.
a. Sheria iliingia ili kosa izidi kuongezeka: Paulo ametuonyesha sheria haituhesabii haki. Sasa anaonyesha yenyewe, sheria haitufanyi sisi kuwa wenye dhambi – Adamu alifanya hivyo. Je, sheria ina lengo gani? Kuna kusudi wazi la sheria na sehemu yake ni ili kosa liwe na wingi. Sheria huifanya dhambi ya mwanadamu kuwa wazi zaidi na zaidi kwa kuitofautisha waziwazi na kiwango cha utakatifu wa Mungu.
i. Mapungufu katika jiwe la thamani huwa mengi yanapolinganishwa na jiwe kamilifu au yanapowekwa kwenye mandhari tofauti. Sheria kamilifu ya Mungu hufichua kasoro zetu, na kufanya dhambi zetu kuwa nyingi.
b. Inaweza kuzidi: Kuna njia nyingine ambayo sheria hufanya dhambi kuzidi. Kwa sababu ya dhambi ya moyo wangu, ninapoona mstari nataka kuuvuka. Kwa maana hii, sheria hufanya dhambi kuwa nyingi kwa sababu huchota mistari iliyo wazi kati ya mema na mabaya ambayo moyo wangu wenye dhambi unataka kuvunja. Kwa hiyo, sheria inanifanya nitende dhambi zaidi – lakini si kwa sababu kuna kitu kibaya katika sheria, lakini kuna kitu kibaya sana katika hali ya kibinadamu.
7. (20b–21) Utawala wa neema.
Wakati dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, nayo neema itawale kwa njia ya haki hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.
a. Dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi: Ikiwa dhambi ilizidi chini ya sheria, neema iliongezeka zaidi chini ya Yesu. Kihalisi, maneno hayo yaliongezeka zaidi yanamaanisha “kuzidi sana.” Mungu hufanya neema yake kuzidi sana, kuwa nyingi kuliko dhambi nyingi!
i. Huenda tulitazamia kwamba pale dhambi ilipozidi, hasira au hukumu ya Mungu ingeongezeka zaidi. Lakini upendo wa Mungu ni wa kustaajabisha sana hata neema ilizidi sana pale ambapo tungetarajia ghadhabu.
ii. Ikiwa neema inazidi juu ya dhambi, basi tunajua dhambi haiwezekani kuzidi neema ya Mungu. Hatuwezi kufanya dhambi zaidi ya vile Mungu anavyoweza kusamehe, lakini tunaweza kukataa neema yake na msamaha wake.
b. Kwa hivyo neema inaweza kutawala: Kama Paulo alivyosema hapo awali, dhambi ilitawala katika kifo. Lakini neema inatawala pia. Utawala wa neema una alama ya haki na uzima wa milele na ni kupitia Yesu.
i. Neema inatawala kwa njia ya haki. Watu wengi wana wazo la neema inapotawala, kutakuwa na kutojali haki na mtazamo wa kawaida kuelekea dhambi. Lakini huo sio utawala wa neema hata kidogo. Paulo aliandika katika waraka mwingine kile neema inatufundisha: Kwa maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa (Tito 2:11–12). Neema inatawala kwa njia ya haki, na neema hufundisha haki.
ii. Neema inatawala hadi kwa uzima wa milele. Neema ya Mungu inatupa kitu na kutupeleka mahali fulani. Inatoa zaidi ya maisha yasiyo na mwisho. Uzima wa milele una wazo la ubora wa sasa wa maisha, ubora wa maisha wa Mungu, tuliopewa sasa hivi – sio tu tunapokufa.
iii. Neema inatawala kupitia Yesu. Kuna Mfalme katika ufalme ambapo neema inatawala, na Mfalme ni Yesu. Maisha ya neema ni juu ya Yesu na wengine, na sio juu yangu. Maisha ya neema haitizami ubinafsi kwa sababu inaelewa kuwa neema isiyostahili kwa Mungu inatolewa na sababu katika nafsi. Sababu zote ziko kwa Yesu; hakuna sababu yoyote ndani yangu. Neema haitawali kupitia nafsi yako, bali kupitia Yesu.
c. Kwa hivyo neema inaweza kutawala kwa njia ya haki: Popote neema inatawala, kiwango cha haki ya Mungu kinaheshimiwa. Hofu ya washika sheria ni utawala wa neema utaipa mioyo miovu kibali cha kutenda dhambi, lakini Maandiko hayashiriki maovu. Neema haikubaliani na dhambi, inakabiliana nayo na kupita dhambi ili kuishinda. Neema haikonyezi udhalimu, inakabiliana na dhambi kwa upatanisho pale msalabani na ushindi uliopatikana kwenye kaburi lililo wazi.
i. Neema si rafiki wa kutenda dhambi; ni adui yake aliyeapishwa. “Kama vile joto hupingana na baridi, na mwanga kwa giza, basi neema ni kinyume na dhambi. Moto na maji vinaweza pia kukubaliana katika chombo kimoja kama neema na dhambi katika moyo huo. (Thomas Benton Brooks)
ii. Katika kitabu cha Pilgrim’s Progress cha kawaida cha John Bunyan, mhusika mzuri anaitwa “Bw. Mwaminifu.” Alisafiri kwa njia ya usafiri na aliona wasfiri wenzake wengi – wengine walitoka kwa ujasiri na kwa nguvu lakini walirudi nyuma. Aliona wengine walijikwaa mwanzoni lakini walimaliza kwa mtindo mzuri. Wengine walianza kujawa na imani lakini waliishia kwa mashaka, na wengine walikuja kupata uhakika zaidi kando ya barabara ya msafiri. Bwana Honest bila shaka alijua mengi kuhusu safari ya maisha ya Kikristo na alijumulisha ujuzi wake wote kwa maneno yake ya mwisho:
“Bw. Honest aliwaita marafiki zake, na kuwaambia ‘Nakufa, lakini sitaacha pendekezo. Kwa habari ya uaminifu wangu, itakwenda pamoja nami’… Ilipofika siku aliyotakiwa kuondoka, alijisemea avuke mto. Sasa mto ule wakati ule ulikuwa umefurika kingo katika sehemu zingine, lakini Bwana Honest katika maisha yake alikuwa amezungumza na mmoja [jina lake] mwenye dhamiri njema kukutana naye huko, na alichofanya pia, akamkabidhi mkono, akamsaidia. yeye juu. Maneno ya mwisho ya Bw. Honest yalikuwa, ‘Neema inatawala!’’ Kwa hiyo aliuacha ulimwengu.”
© 2024 The Enduring Word Bible Commentary by David Guzik – [email protected]