Warumi 2 – Hatia ya Mwenye Maadili na Myahudi
A. Hukumu ya Mungu juu ya walioelimika kiadili.
1. (1–3) Shitaka dhidi ya mtu aliyeelimika kiadili.
Huna udhuru, ee mwanadamu, ye yote umhukumuye; ninyi mnaohukumu mnafanya yale yale. Lakini tunajua kwamba hukumu ya Mungu ni ya kweli dhidi ya wale wanaofanya mambo kama hayo. Na wewe, unayewahukumu watu wafanyao hayo na unayafanya yale yale, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu?
a. Kwa hiyo huna udhuru, ewe mwanadamu, ye yote umhukumuye: Katika Warumi 1, Paulo alionyesha dhambi ya wenye hatia mbaya sana. Sasa anazungumza na wale ambao wana maadili katika mwenendo wao. Paulo anawachukulia kuwa wanajipongeza kwamba wao si kama watu walioelezwa katika Warumi 1.
i. Mfano mzuri wa wazo hili ni mfano wa Yesu wa Mfarisayo na Mtoza ushuru. Tukichukua kutoka kwa mfano wa Yesu, Paulo alizungumza na Mtoza ushuru katika Warumi 1 na sasa anazungumza na Mfarisayo (Luka 18:10–14).
ii. Wengi miongoni mwa watu wa Kiyahudi wa siku za Paulo walifananisha maadili; lakini maneno yake katika Warumi 2:1–16 yanaonekana kuwa na matumizi mapana. Kwa mfano, kulikuwa na Seneca, mwanasiasa wa Kirumi, mwalimu wa maadili na pia mwalimu wa Nero. Angekubaliana kwa kauli moja na Paulo kuhusu maadili ya wapagani wengi, lakini mtu kama Seneca angedhania, “mimi ni tofauti na wale watu hao wasio na maadili.”
iii. Wakristo wengi walipendzwa na Seneca na msimamo wake thabiti wa “maadili” na “thamani ya familia.” Lakini mara nyingi alivumilia maovu ambayo hayakuwa tofauti na yale ambayo aliyashutumu kwa wengine – mfano wa wazi zaidi ukiwa ni uhusiano wake Nero katika mauaji ya mama yake Agrippina. (Bruce)
b. Katika jambo lolote unalomhukumu mwingine unajihukumu mwenyewe: Baada ya kupata makubaliano ya wenye maadili kumhukumu mwenye dhambi, sasa Paulo anageuza hoja iyo hiyo juu ya mwenye maadili. Hii ni kwa sababu mwisho wa yote, ninyi mnaohukumu mnafanya mambo yale yale.
i. Tunapomhukumu mtu mwingine, tunaelekeza kiwango nje ya nafsi yetu – na kiwango hicho kinamhukumu kila mtu, sio tu mwenye dhambi wa dhahiri.Kwa kuwa unajua haki ya Mungu, kama inavyothibitishwa na ukweli ya unahukumu wengine, huna kisingizio, kwa sababu katika tendo lile la kuhukumu umejihukumu mwenyewe. (Murray)
ii. Mazoezi ya mambo yale yale: Ona kwamba mwenye maadili hahukumiwi kwa kuwahukumu wengine bali kwa hatia ya mambo yale yale anayowahukumu wengine. Hili ni jambo ambalo mtu mwenye maadili angepinga (“Mimi si kama wao hata kidogo!”), lakini Paulo atadhihirisha hili ni kweli.
iii. Wuest, akimnukuu Denney wewe unayehukumu unafanya mambo yale yale: “Mnatenda yale wanayo tenda, lakini mwenendo wenu ni sawa, kwa mfano, mnatenda dhambi dhidi ya nuru. Dhambi ya Wayahudi ilikuwa sawa, lakini matendo yao sio.”
c. Kulingana na ukweli: Hili lina wazo la “kulingana na ukweli wa kesi.” Mungu atahukumu (na kulaani) mwenye maadili kwa ukweli.
d. Jambo hilo limewekwa wazi: ikiwa mwenye maadili ana hatia sawa na mwenye dhambi wataepukaje hukumu ya Mungu?
i. Wewe unasisitiza katika swali, “[unafikiri] wewe utaepuka hukumu ya Mungu?” Paulo anayabeba ya hapa chini, akiruhusu msomaji wake kujua kwamba yeye hajaachwa nje ya kanuni hii. Paulo alijua jinsi ya kufikia mioyo ya wasomaji wake. “Mawaidha yetu yanapaswa kuwa kama mishale iliyochongwa na kushika mioyo ya watu, wala si jeraha tu, kama mishale mingine.” (Trapp)
ii. Lenski juu ya mwadilifu: “Lengo la Paulo ni kubwa zaidi kuliko hukumu na udhalimu. Anawanyang’anya,na lazima awanyang’anye, mwenendo wao wa uadilifu kwa sababu wanaiona hii kama njia ya kuepuka ghadhabu ya Mungu.
2. (4–5) Hukumu ya Mungu dhidi ya waadilifu inatangazwa.
Au wadharau wingi wa wema wake, ustahimilivu wake, na uvumilivu wake, pasipo kujua kwamba wema wa Mungu unakuelekeza kutubu? Na kwa kadiri ya ugumu wako, na moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya ghadhabu katika siku ya ghadhabu na ufunuo wa hukumu wa haki ya Mungu,
a. Au unadharau wingi wa wema wake, ustahimilivu wake, na unyenyekevu wake katika mateso yake: Paulo anaonyesha kwamba mwenye maadili mwenyewe hudharau wema, ustahimilivu, na uvumilivu wa Mungu, ambao wote wanapaswa kuwaleta wenye maadili katika toba ya unyenyekevu badala ya mtazamo wa ubora.
i. Wema unaweza kuchukuliwa kuwa fadhili za Mungu kwetu kuhusiana na dhambi zetu za zamani. Amekuwa mwema kwetu kwa sababu vado hajatuhukumu ingawa tunastahili.
ii. Ustahimilivu unaweza kuchukuliwa kama wema wa Mungu kwetu kuhusiana na dhambi zetu za sasa. Leo hii – hakika, wakati huu – tumepungukiwa na utukufu wake, lakini anazuia hukumu yake dhidi yetu.
iii. Mateso mengi inaonekana kuwa fadhili za Mungu kwetu kuhusiana na dhambi yetu ya wakati ujao. Anajua tutatenda dhambi kesho na kesho kutwa, lakini anazuia hukumu yake dhidi yetu.
iv. Tukizingatia haya yote, haishangazi kwamba Paulo anaeleza sifa hizi tatu za wema za Mungu kwetu kama utajiri. Utajiri wa rehema za Mungu unaweza pimwa kwa mambo manne:
∙ Ukuu wake – kumkosea mtu mkuu ni kosa kubwa na Mungu ni mkuu kuliko yote – lakini anaonyesha huruma.
∙ Ujuzi wake wa kujua yote – ikiwa mtu angejua dhambi zetu zote, wangeonyesha huruma? Hata hivyo Mungu huonyesha rehema.
∙ Nguvu zake – wakati mwingine makosa hayatatuliwi kwa sababu yako nje ya uwezo wetu, lakini Mungu anaweza kusuluhisha kila uovu dhidi yake – lakini Yeye ni mwingi wa rehema.
∙ Mlengwa wa rehema yake: Mwanadamu – Je,tungeonyesha huruma kwa siafu? Lakini Mungu ni mwingi wa rehema.
v. Tukijua jinsi wema wa Mungu ulivyo mkuu, ni dhambi kuu kudharau fadhili za Mungu, na kwa urahisi tunafikia kuamini kwamba tunastahili.
b. Uvumilivu na ustahimilivu: Wanadamu mara nyingi hufikiria hii kama udhaifu wa Mungu. Wanasema mambo haya “Ikiwa kuna Mungu mbinguni, na aniangamishe nife!” Wakati halijatokea, watasema, “Tazama, nilikuambia hakuna Mungu.” Wanadamu wanatafsiri vibaya ustahimilivu wa Mungu na upole wake kuwa ni kibali chake, na wanakataa kutubu.
i. “Ninaona ya kuwa kila asubuhi mtu anapoamka bado hajatubu, na kujikuta nje ya kuzimu, mwanga wa jua unaonekana kusema, ‘Ninakuangazia siku nyingine tena, ili katika siku hii upate kutubu.’ Wakati kitanda chako kinapokupokea usiku nadhani kinaonekana kusema, ‘Nitakupa pumziko la usiku mwingine, ili uishi uziache dhambi zako na kumtumaini Yesu.’ Kila mkate uletao kweny meza unasema, ‘Nina budi kuutegemeza mwili wako ili upate nafasi ya kutubu.’ Kila unapofungua Biblia kurasa husema, ‘Tunazungumza nawe ili upate kutubu.’ Kila mara unaposikia mahubiri, yakiwa ni mahubiri ambayo Mungu angependa tuhubiri, yanakusihi umgeukie Bwana na kuishi.” (Spurgeon)
c. Pasipo kujua wema wa Mungu unakuongoza upate kutubu: Watu wengi hawaelewi wema wa Mungu kwa waovu. Hawaelewi sababu yake ni kuwaongoza kwenye toba.
i. Wanadamu waone wema wa Mungu na waelewe:
∙ Mungu amekuwa bora kwao kuliko walivyostahili.
∙ Mungu amewafanyia wema walipompuuza.
∙ Mungu amewafanyia wema walipomdhihaki.
∙ Mungu si bwana katili na wanaweza kujisalimisha kwake wakawa salama.
∙ Mungu yuko tayari kabisa kuwasamehe.
∙ Mungu anapaswa kutumikiwa kwa shukrani sahihi.
ii. Je, unangoja Mungu akulazimishe kwenye toba? Yeye hafanyi hivyo; Mungu anakuongoza kwenye toba.“Angalieni, wapendwa, Bwana hawalazimishi kutubu. Kaini alifukuzwa kama mtoro na mzururaji, alipomwua Abeli ndugu yake mwadilifu; Yuda akaenda na kujinyonga, akiongozwa na uchungu wa kujuta kwa sababu ya yale aliyoyafanya kwa kumsaliti Bwana wake; lakini toba iliyo tamu na iliyo bora zaidi ni ile inayokuja, si kwa kushurutishwa, bali kwa kuvutwa: ‘Wema wa Mungu unakuongoza kwenye toba.’” (Spurgeon)
iii. “Katika Agano Jipya, toba si hasi tu. Inamaanisha kugeukia maisha mapya katika Kristo, maisha ya utumishi kwa Mungu. Haipaswi kuchanganyishwa na majuto, ambayo ni huzuni kubwa kwa ajili ya dhambi lakini haina maelezo ya toba.” (Morris)
d. Unajiwekea akiba ya ghadhabu kwa siku ya ghadhabu na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu: Kwa sababu ya dhana juu ya neema ya Mungu, Paulo anaweza kusema kwa usahihi kwamba mwenye maadili anajiwekeahazina … hasira katika siku ya ghadhabu.
i. Mtaalamu wa maadili hufikiri anaweka hazina kwa Mungu anapowashutumu “wenye dhambi” wanaomzunguka. Kwa kweli, yeye huweka ghadhabu ya Mungu tu. “Kama watu wanavyo ongeza hazina zao za mali, ndivyo unavyo wekeza hazina za ghaadhabu kwenye hukumu yako.” (Poole)
ii. Wanadamu wanapoweka hazina ya ghadhabu kwa Mungu dhidi yao, ni nini kinachozuia gharika ya ghadhabu? Mungu Mwenyewe! Anazuia kutokana na upole wake na uvumilivu wake! “Ni mzigo ambao Mungu hubeba, ambao wanadamu hurundika zaidi na zaidi, na kufanya kuwa mzito na mzito zaidi. Ajabu ya hayo yote ni kuwa Mungu hashikili hayo hata kwa siku moja; lakini yeye hushikilia uzito huo wote, wala hauanguki juu ya kichwa cha mwenye dhambi.” (Lenski)
e. Katika siku ya ghadhabu na ufunuo wa hukumu ya haki kutoka kwa Mungu: Katika ujio wa kwanza wa Yesu sifa ya upendo wa Mungu ilifunuliwa kwa msisitizo mkubwa zaidi. Katika ujio wa pili wa Yesu hukumu ya haki ya Mungu itafunuliwa kwa uwazi zaidi.
3. (6–10) Mungu atawahukumu wenye maadili kwa sababu matendo yao pia yanapungukiwa na kiwango kamilifu cha Mungu.
Nani “atamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”: uzima wa milele kwa wale hudumu katika kutenda mema wanatafuta utukufu, heshima, na kutokufa; bali na wale wabinafsi, na wasioitii ukweli, bali wanatii udhalimu; ghadhabu na dhiki juu ya kila nafsi ya mtu atendaye maovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; bali utukufu,heshima na amani kwa kila atendaye mema, kwa Myahudi kwanza na Myunani.
a. Atamlipa kila mmoja kadiri ya matendo yake: Hili ni wazo la kutisha na la kuogofya, linamhukumu mwenye maadili na mtenda dhambi.
b. Uzima wa Milele kwa wale: Ikiwa mtu kwa dhati alifanya mema wakati wote, angeweza kustahili uzima wa milele kwa hiari yake mwenyewe – lakini hakuna, kwa sababu wote, kwa namna fulani au nyingine, wamekuwa, au watakuwa na watanafisi na kufanya,kutotii ukweli, na kutii udhalimu.
c. Mahangaiko na ghadhabu, dhiki na vitisho, juu ya kila nafsi ya mwanadamu anayetenda maovu: Kwa sababu wote wanapungukiwa na kiwango hiki cha wema wa kudumu wa Mungu, ghadhabu ya Mungu itawajia wote watendao maovu – bila kujali kama ni Myahudi au Mmataifa.
i. Hukumu hii inamjia Myahudi kwanza. Ikiwa wao ni wa kwanza katika mstari wa injili (Warumi 1:16) na wa kwanza katika mstari wa taji (Warumi 2:10), basi wao pia ni wa kwanza kwenye mstari wa hukumu.
ii. Neno kukasirika linatokana na wazo la “kuchemka,” maana yake mlipuko wa shauku. Neno ghadhabu linatokana na wazo la uvimbe ambao hatimaye hupasuka, na linatumika zaidi kwa hasira inayotokana na mtu aliyetulia.
B. Hukumu ya Mungu juu ya mtu wa Kiyahudi.
1. (11–13) Kanuni ya Mungu ya kutobagua.
Kwa kuwa hakuna upendeleo kwa Mungu. Kwa wote waliokosa pasipo sheria wataangamia pasipo sheria; na wote waliokosa kwenye sheria, watahukumiwa kwa sheria, (sio waielewao sheria walio waadilifu mbele za Mungu, bali ni waitendao sheriawatahesabiwa haki;
a. Hakuna upendeleo kwa Mungu: Neno lililotafsiriwa upendeleo linatokana na maneno mawili ya kale ya Kiyunani – kupokea na kukabili. Ina maana ya kuhukumu mambo kwa misingi ya nje au mawazo yaliyotungwa.
i. Baadhi ya marabi wa kale walifundisha kwamba Mungu alionyesha upendeleo kwa Wayahudi, walisema: “Mungu atawahukumu Mataifa kwa kipimo kimoja na Wayahudi kwa kipimo kingine.”
b. Kwa maana siwaielewao sheria ya Mungu pekee yao ni wenye haki machoni pa Mungu, bali waitendao sheria pia watahesabiwa haki Hukumu ya haki ya Mungu haizuiliwi kwa sababu mtu ameisikia sheria, inazuiliwa tu kama mtu anatimiza sheria.
i. Myahudi – au mtu wa dini – anaweza kufikiri ameokoka kwa sababu anayo sheria, lakini je, ameielewa? Mtu wa mataifa anaweza kufikiri ameokoka kwa sababu hana sheria, lakini je, ameshika maagizo ya dhamiri yake mwenyewe?
ii. Watu watahukumiwa, si kwa sababu wana sheria au hawana sheria, bali kwa sababu wamefanya dhambi. (Morris)
c. Wote waliotenda dhambi pasipo sheria wataangamia pasipo sheria: Hukumu ya dhambi inaweza kuja pamoja na sheria au pasipo sheria.
2. (14–16) Kumiliki sheria si faida kwa Myahudi katika Siku ya Hukumu.
Wakati watu wa mataifa, wasio na sheria, kwa tabia zao wanayafanya yaliyo katika torati, wajapokuwa hawana sheria ni sheria kwao yao, waionyeshao kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao. Dhamiri ikiwashuhudia, na mawazo yao kati yao ikiwashitaki au kuwatetea) katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa Yesu Kristo, kadiri ya injili yangu.
a. Ingawa kutokuwa na sheria, ni sheria kwao wenyewe: Paulo anaeleza kwa nini Mmataifa anaweza kuhukumiwa bila sheria. Dhamiri yao (ambayo ni kazi ya sheria iliyoandikwa mioyoni mwao) inatosha kuwahukumu – au, kinadharia sheria hii juu ya moyo inatosha kuwahalalisha.
i. Imeandikwa mioyoni mwao: Waandishi wengi wa kipagani wa siku za Paulo walirejelea “sheria isiyoandikwa” ndani ya mwanadamu. Walilifikiria kuwa jambo ambalo lilielekeza mwanadamu kwenye njia sahihi. Ingawa haijajumuishwa kwa sheria zilizoandikwa, kwa upande mwingine ni muhimu zaidi kuliko sheria iliyoandikwa.
ii. Sheria zao wenyewe haimaanishi hawa “Mataifa watiifu” walitunga sheria yao wenyewe (kama tunavyotumia usemi “sheria kwake”), bali walikuwa watiifu kwa dhamiri, kazi ya sheria iliyokaa ndani yao wenyewe.
iii. “Yeye aonyesha ujinga unafanywa kuwa kisingizio bure na watu wa mataifa mengine, kwa kuwa wanathibitisha kwa matendo yao kwamba wana kanuni ya uadilifu.” (Calvin)
b. Mawazo yao yakiwashutumu au kuwasamehe: Kinadharia, mtu anaweza kuhesabiwa haki (“kusamehewa”) kwa kutii dhamiri yake. Kwa bahati mbaya, kila mwanadamu amekiuka dhamiri yake (ufunuo wa ndani wa Mungu kwa mwanadamu), kama vile kila mwanadamu amekiuka ufunuo ulioandikwa wa Mungu.
i. Paulo anasema katika Warumi 2:14 kwamba mtu wa Mataifa, anaweza kwa asili kufanya mambo yaliyomo katika sheria yeye ni mwangalifu asiseme kwamba mtu wa mataifa anaweza kutimiza matakwa ya sheria kikamilifu.
ii. Ingawa Mungu ana kazi Yake ndani ya kila mwanadamu (iletayo dhamiri), mwanadamu anaweza kufisidi kazi hiyo, ili dhamiri itofautiane kati ya mtu na mwingine. Tunajua pia dhamiri yetu inaweza kuharibika kwa njia ya dhambi na uasi, lakini inaweza kurejeshwa katika Yesu.
iii. Ikiwa dhamiri yetu inatuhukumu kimakosa, tunaweza kufarijiwa na wazo la Mungu ni mkuu kuliko moyo wetu (1 Yohana 3:20).
c. Dhamiri zao pia ni shahidi: Watu ambao hawajawahi kusikia neno la Mungu wana dira ya maadili wanayowajibika kwayo – dhamiri.
i. Mungu anaeleza jinsi Alivyowaumba watu wote: kuna ‘kazi’ ndani yao, inayowafanya wawe na ufahamu wa maadili.(newelli)
ii. “Hasemi torati imeandikwa mioyoni mwao kama watu wasemavyo mara nyingi; bali kazi ya torati, yale matakwa ya sheria kwa wanadamu, yameandikwa humo. (Morris)
d. Siku ambayo Mungu atahukumu: Siku hii hakuna mtu atakayeepuka hukumu ya Mungu kwa kudai kutojua ufunuo Wake ulioandikwa. Kukiuka ufunuo wa ndani wa Mungu kunatosha kutuhukumu sisi sote.
i. “Basi Mungu atayahukumu mataifa yote, kulingana na matumizi na matusi waliyoyatumia kwa neno hili, kama limeandikwa moyoni, au limeandikwa katika mbao za mawe. (Clarke)
e. Kulingana na injili yangu: Ona siku ya hukumu ilikuwa sehemu ya injili ya Paulo. Hakusitasita kutangaza uwajibikaji kamili wa mwanadamu kwa Mungu.
i. “’Injili yangu.’ Je, hili halionyeshi ujasiri wake? Hata kusema, siionei haya Injili; ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye. Anasema, ‘injili yangu,’ kama askari anavyozungumza kuhusu ‘rangi yangu,’ au ya ‘mfalme wangu.’ Anaazimia kuubeba bendera hii kwa ushindi, na kutumikia ukweli huu wa kifalme hata kifo. (Spurgeon)
f. Mungu atazihukumu siri za wanadamu kwa Yesu Kristo: Dhana hii ya Kikristo. Wayahudi walifundisha kwamba Mungu Baba pekee ndiye atakayehukumu ulimwengu, asitoe hukumu kwa yeyote – hata Masihi.
3. (17-20) Kujisifu kwa Myahudi.
Hakika wewe unaitwa Myahudi, na kutulia juu ya sheria, na kujisifu katika Mungu, na kuyajua mapenzi yake, na kuyahalalisha yaliyo mema, ukiyaagiza kutokana na sheria na kujua hakika wewe ni kielelezo wa vipofu, nuru kwa walio gizani, mwaashiri wa wapumbavu, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na kweli katika torati.
a. Hakika wewe unaitwa Myahudi, na unaiegemea sheria: Kila “kujisifu” kwa Myahudi katika kifungu hiki kinahusu kuwa na sheria. Wayahudi wa siku za Paulo walikuwa na kiburi na uhakika kuwa Mungu aliwapa sheria yake takatifu kama taifa. Waliamini hili ni thibitisho la hali yao ya kuwa watu maalum waliochaguliwa, na hiyo kuwa hakikisho ya wokovu wao.
b. Kuwa na ujuzi: Ingawa Myahudi anapaswa kupokea sheria kwa shukrani kama zawadi kutoka kwa Mungu, Paulo ataonyesha jinsi kuwa na sheria tu hauwezeshi mtu kuwa wa haki.
4. (21–24) Shitaka dhidi ya Myahudi.
Basi wewe unayemfundisha mwingine, je, hujifundishi mwenyewe? Wewe unayehubiri mtu asiibe, je, unaiba? Wewe unayesema, “Usizini,” je, unazini? Wewe unayechukia sanamu, unaiba mahekalu? Wewe unayejivunia sheria, je, unamvunjia Mungu heshima kwa kuivunja sheria? Kwa maana jina la Mungu linatukanwa kati ya mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.
a. Kwa hiyo, wewe unayemfundisha mwingine, hujifundishi mwenyewe? Inakuja kwenye kanuni hii: “Wewe unayo sheria, Unaweza kuona jinsi wengine wanavyovunja sheria, unaona jinsi unavyoivunja pia?”
i. Sehemu kubwa ya Dini ya Kiyahudi wa marabi ya siku za Paulo walitafsiri sheria wakifikiri kwamba walikuwa wamehesabiwa haki katika sheria. Yesu alifichua makosa ya tafsiri hizo (Mathayo 5:19–48).
ii. Mungu hutumia sheria yake kwa matendo yetu na mitazamo yetu. Wakati mwingine tunataka tu mitazamo yetu itathminiwe, na wakati mwingine matendo yetu tu. Mungu atatuwajibisha kwa nia na matendo.
iii. “Wanafiki wanaweza kuzungumza juu ya dini, kana kwamba ndimi zao zilifuatana na mifano, wao ni maprofesa wazuri, lakini wakosefu; alivyokuwa yule kardinali Cremensia wa kimwili, mjumbe wa papa, aliyetumwa hapa, BK 1114, kuzuia ndoa za mapadre, na kuchukuliwa katika tendo hilo kwa tarumbeta ya kawaida, aliisamehe kwa kusema yeye si kuhani mwenyewe, bali mrekebishaji wao.” (Trapp)
b. Ninyi mnaochukia sanamu, mnaiba mahekalu: Morris anazungumza wazo la kuiba mahekalu. “Ni wazi kuwa watu fulani waliamini kwamba Myahudi angeweza kupata faida kutokana na mazoea ya kukosa unyoofu yanayohusiana na ibada ya sanamu, na huenda Paulo alikuwa akifikiria jambo hilo.”
c. Jina la Mungu linatukanwa kati ya mataifa kwa ajili yenu: Paulo anamkumbusha wayahudi Mungu alisema katika Agano la Kale kushindwa kwa Wayahudi kutii sheria kunasababisha watu wa mataifa mengine kumkufuru Mungu.
5. (25–29) Kutokuwa na maana kwa kutahiriwa.
Kutahiriwa kwafaa kama unatii sheria; lakini ikiwa wewe ni mvunja sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. Kwa hiyo, ikiwa mtu asiyetahiriwa anashika matakwa ya uadilifu wa sheria, je, kutotahiriwa kwake kutahesabiwa kuwa kutahiriwa? Na je, yule asiyetahiriwa kimwili, akiitimiza sheria, hatakuhukumu wewe ambaye, hata kwa sheria yako iliyoandikwa ya kutahiriwa, unaivunja sheria? Maana yeye si Myahudi kwa nje, wala tohara si ile ionekanayo tu katika mwili; bali yeye ni Myahudi aliye ndani; na tohara ni ya moyo, katika Roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
a. Kwa maana kutahiriwa kwafaa kweli ukishika sheria: Paulo anatambua kwamba Myahudi anaweza kupinga na kusema kwamba wokovu wake unatokana na ukweli yeye ni mzao wa Abrahamu, aliyethibitishwa kwa tohara. Paulo anajibu kwa usahihi hili halina umuhimu kuhusiana na kuhesabiwa haki.
i. Myahudi aliamini kutahiriwa kwake kulimhakikishia wokovu wake. Anaweza kuadhibiwa katika ulimwengu ujao, lakini asingeweza kupotea kamwe.
ii. Katika siku za Paulo, marabi fulani walifundisha kwamba Abrahamu aliketi kwenye mlango wa kuzimu na kuhakikisha hakuna uzao wake wowote aliyetahiriwa anaeenda huko. Baadhi ya Marabi pia walifundisha “Mungu atawahukumu Mataifa kwa kipimo kimoja na Wayahudi kwa kipimo kingine” na “Waisraeli wote watakuwa na sehemu katika ulimwengu ujao.” (Barclay)
iii. Tohara (au ubatizo – au tambiko lolote lenyewe)haimwokoi mtu yeyote. Katika ulimwengu wa kale Wamisri pia waliwatahiri wavulana wao lakini haikuwafanya wawe wafuasi wa Mungu wa kweli. Hata katika siku za Ibrahimu Ishmaeli (mwana wa kimwili) alitahiriwa, lakini haikumfanya kuwa mwana wa agano.
iv. Tohara na ubatizohufanya kwa usawa kile ambacho lebo ufanya kwenye mkebe. Ikiwa lebo ya nje hailingani na iliyo ndani, kuna kitu kibaya! Ikiwa kuna karoti ndani ya kopo, unaweza kuweka lebo inayosema “Peas” lakini haibadilishi kilicho ndani ya kopo. Kuzaliwa mara ya pili hubadilisha kile kilicho ndani ya mkebe, na kisha unaweza kuweka lebo ifaayo nje.
v. Bila shaka, hili si wazo jipya. Sheria ya Musa yenyewe inafundisha kanuni hii: Basi zitahiriwe govi za mioyo yenu, wala msiwe wakaidi tena (Kumbukumbu la Torati 10:16).
b. Kwa hiyo, ikiwa mtu asiyetahiriwa atayashika matakwa ya haki ya torati: Ikiwa mtu wa Mataifa angeshika matakwa ya haki ya sheria kwa dhamiri yake (Warumi 2:15 inavyoonyesha), asingehesabiwa haki, badala ya Myahudi aliyetahiriwa nani hakushika sheria? Jambo linasisitizwa, kuwa na sheria au kufanya sherehe haitoshi. Mungu anataka haki.
i. Morris akimnukuu Mansoni: “Ikiwa ni waaminifu kwa mema wanayojua, watakubaliwa na Mungu; basi ni ‘ikiwa’ kubwa sana.”
c. Na yule asiyetahiriwa kimwili, akiitimiza sheria, hatakuhukumu wewe ambaye, hata kwa sheria yako iliyoandikwa na kutahiriwa, u mvunja sheria? Hili ndilo jibu la Mungu kwa yule anayesema, “Na Je! kuhusu Mbilikimo wa Afrika ambao hawajawahi sikia injili?” Mungu atamhukumu Mbilikimo huyo kwa yale aliyoyasikia, na jinsi ameishi nayo. Bila shaka, hii ina maanisha Mbilikimo watakuwa na hatia mbele za Mungu, kwa sababu hakuna mtu ambaye ameishi kikamilifu kwa dhamiri yake, au ameitikia kikamilifu kile tunachoweza kujua kuhusu Mungu kupitia uumbaji.
i. Tatizo la “mzawa asiye na hatia” hatuwezi kupata mzaliwa asiye na hatia popote.
ii. “Na Je! Mbilikimo katika Afrika ambao hawajasikia injili?” ni swali zuri, lakini kuna maswali mawili muhimu zaidi:
∙ Je, wewe unayesikia injili, lakini unaikataa? Je, kuna kisingizio gani kwako?
∙ Je wewe, ambaye umeamriwa kupeleka injili kwa Mbilikimo huko Afrika (Mathayo 28:19), lakini unakataa?
d. Sifa Zake hazitoki kwa watu ila kwa Mwenyezi Mungu. Ishara zote nje ya dini zinaweza kutupatia sifa kutoka kwa watu, lakini hazitatupatia sifa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Uthibitisho wa haki yetu kwa Mungu haumo katika ishara ya nje au kazi, na hauhakikishwi kwa sababu ya uzazi wetu. Ushahidi unapatikana katika kazi ya Mungu ndani ya mioyo yetu inayojionyesha yenyewe katika mazao.
e. William Newelli anatoa muhtasari wa Warumi 2 na “Kanuni Saba Kuu za Hukumu ya Mungu” ambazo zinafaa kuzingatiwa:
∙ Hukumu ya Mungu ni kulingana na ukweli (Warumi 2:2).
∙ Hukumu ya Mungu ni kulingana na hatia iliyokusanywa (Warumi 2:5).
∙ Hukumu ya Mungu ni kwa matendo (Warumi 2:6).
∙ Hukumu ya Mungu haina upendeleo (Warumi 2:11).
∙ Hukumu ya Mungu ni kulingana na utendaji, sio ujuzi (Warumi 2:13).
∙Hukumu ya Mungu huzifikia siri za moyo (Warumi 2:16).
∙ Hukumu ya Mungu ni kulingana na uhalisia, si matamshi ya kidini (Warumi 2:17–29).
© 2024 The Enduring Word Bible Commentary by David Guzik – [email protected]