Warumi 1 – Jamii ya Wanadamu Wana Hatia Mbele za Mungu
A. Umuhimu na athari ya Waraka wa Paulo kwa Warumi.
1. Athari ya Warumi kwa Augustino.
a. Katika msimu wa joto wa 386, kijana alilia nyuma ya jumba la rafiki yake. Alijua maisha yake ya dhambi na uasi dhidi ya Mungu yalimwacha mtupu na kujisikia kufa; lakini hakuweza kupata nguvu ya kufanya uamuzi wa mwisho, wa kweli kwa Yesu Kristo. Alipokuwa ameketi, alisikia watoto wakicheza na waliitana maneno haya: “Chukua usome! Chukua na usome!”
b. Akifikiri kwamba Mungu alikuwa na ujumbe kwake kupitia maneno ya hao watoto, aliichukua gombo lililokuwa karibu na akaanza kulisoma: si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo na msitoe nafasi kwa miili yenu kutimiza tamaa zake (Warumi 13:13b–14). Hakuendelea kusoma, haikuwa lazima. Kupitia uwezo wa neno la Mungu, Agustino wakati huo alipata imani ya kutoa maisha yake yote kwa Yesu Kristo.
2. Athari ya Warumi kwa Martin Luther.
a. Mnamo Agosti 1513, mtawa alitoa hotuba ya Kitabu cha Zaburi kwa wanafunzi wa seminari, lakini maisha yake ya ndani hayakuwa chochote ila masikitiko. Katika masomo yake alikutana na Zaburi 31:1: Kwa haki yako unikomboe. Kifungu hicho kilimchanganya Luther; uadilifu wa Mungu aingewezaungeweza kufanya nini isipokuwa kumhukumu kwenda jehanamu kama adhabu ya haki kwa ajili ya dhambi zake? Luther aliendelea kuwaza kuhusuWarumi 1:17, isemayo: haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani, kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani.
b. Mtawa Luther aliendelea kusema: “Usiku na mchana nilitafakari mpaka… nikafahamu ukweli kwamba haki ya Mungu ni ile haki ambayo ni, kwa neema na rehema, anatuhesabia haki kwa imani. Kwa hivyo nilijiisi nimezaliwa upya na kupitia mlango iliyofunguliwa hadi paradiso… Kifungu hiki cha Paulo kilikuwa kwangu lango wa kuingia mbinguni.” Martin Luther alizaliwa mara ya pili, na Matengenezo ya Kanisa yakaanza moyoni mwake.
3. Athari ya Warumi kwa John Wesley.
a. Mnamo Mei 1738, mhudumu na mmishonari aliyeshindwa kwa kusita alienda kwenye somo dogo la Biblia ambapo mtu fulani alisoma kwa sauti kutoka katika maoni ya Martin Luther juu ya Warumi.
b. Kama vile Wesley, yule mmishonari aliyeshindwa, alisema baadaye: “Alipokuwa akielezea badiliko ambalo Mungu anafanya moyoni kupitia imani katika Kristo, nilihisi moyo wangu ukiwa na joto la ajabu. Nilihisi nilimwamini Kristo, Kristo pekee, kwa ajili ya wokovu wangu, na uhakikisho nilipewa kwamba alikuwa ameondoa dhambi zangu, hata zangu.” John Wesley aliokolewa usiku huo huko London.
4. Zingatia ushuhuda wa watu hawa kuhusu Warumi:
a. Martin Luther aliwasifu Warumi: “Ni sehemu muhimu ya Agano Jipya na injili kamilifu… kielelezo kamili cha injili.”
b. Mrithi wa Luther, Philip Melanchthon aliwataja Warumi, “Mkusanyiko wa mafundisho ya Kikristo.”
c. John Calvin alisema hivi kuhusu Kitabu cha Warumi, “Mtu yeyote anapoielewa Waraka huu, ana kifungu kilichofunguliwa kwake ili apate kuelewa Maandiko yote.”
d. Samuel Coleridge, mshairi wa Kiingereza na mkosoaji wa fasihi alisema barua ya Paulo kwa Warumi ni “Kazi ya kina zaidi kuwepo.”
e. Frederick Godet, mwanatheolojia wa Uswizi wa Karne ya 19 alikitaja Kitabu cha Warumi “Kanisa kuu la imani ya Kikristo.”
f. G. Campbell Morgan alisema Warumi “ulikuwa ukurasa wa fasihi unaotamanisha zaidi ambao macho yako yameona na wakati uo huo, shairi la matumaini zaidi ambalo masikio yako yamewahi kusikiliza.”
g. Richard Lenski aliandika kwamba Kitabu cha Warumi “bila shaka ndiyo barua yenye ubora zaidi miongoni mwa barua zote za Agano Jipya hata kama ilivyoandikwa kwenye kilele cha kazi ya kitume ya Paulo.”
5. Tunapaswa pia kukumbuka maneno ya Mtume Petro kuhusu barua ya Paulo: Pia ndugu wetu mpendwa Paulo amewaandikia kwa hekima aliyopewa, kama vile katika nyaraka zake zote… ambamo ndani yake mna mambo fulani magumu kueleweka (2 Petro 3:15–16).
a. Kitabu cha Warumi kina ukweli unaobadilisha maisha, lakini ni lazima ufikiwe kwa juhudi na dhamira ili kuelewa kile ambacho Roho Mtakatifu alisema kupitia kwa Mtume Paulo
B. Utangulizi.
1. (1) Paulo anajitambulisha kwa Wakristo wa Kirumi.
Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, aliyetengwa kwa injili ya Mungu
a. Paulo: Maisha na huduma ya Mtume Paulo (anayejulikana pia kama Sauli wa Tarso) yameandikwa vyema katika Matendo sura ya 8 hadi 28, pamoja na Wagalatia 1 na 2, na 2 Wakorintho 11 na 12.
i. Inakaribia kuafikiwa kote ulimwenguni kwamba Paulo aliandika Warumi kutoka mji wa Korintho alipokaa huko katika majira ya baridi katika safari yake ya tatu ya umishonari kama ilivyoelezwa katika Matendo 20:2–3. Hili linatokana na Warumi 16:1 na 16:23 pamoja na 1 Wakorintho 1:14. Wachambuzi mbalimbali huchagua tarehe ya kuandikwa popote kuanzia BK 53 hadi 58.
ii. Paulo alipoandika Kitabu cha Warumi, alikuwa tayari amekua mhubiri wa Mkristo kwa takriban miaka 20. Akiwa njiani kuelekea Yerusalemu, alikuwa na miezi mitatu huko Korintho bila shughuli zingine. Aliwazia wakati huu kama wakati mzuri wa kuwaandikia mapema Wakristo wa Roma, kanisa alipanga kutembelea baada ya safari ya kwenda Yerusalemu.
iii. Paulo alipojaribu kwenda Roma, Roho Mtakatifu alimwonya kuhusu hatari iliyokuwa ikimngojea huko Yerusalemu (Matendo 21:10–14). Je, kama hangeweza kufika Roma? Hivyo ilimlazimu awaandikia barua yenye maelezo mengi sana, hivi kwamba Wakristo wa Rumi walikuwa na injili aliyohubiri Paulo, hata kama Paulo mwenyewe hakuweza kuwatembelea.
iv. Kwa sababu ya haya yote, Warumi ni tofauti kushinda nyingi za barua ambazo Paulo aliyaandikia makanisa. Barua zingine za Agano Jipya zinalenga zaidi kanisa na changamoto pamoja na matatizo yao. Barua kwa Warumi inalenga zaidi juu ya Mungu na mpango wake mkuu wa ukombozi.
v. Tunajua Waraka kwa Warumi ulithaminiwa na Wakristo wa Rumi; Klementi kwa barua ya Rumi katika mwaka wa BK 96 anaonyesha ujuzi mkubwa wa barua ya Paulo. Huenda ikawa kwamba aliikariri na kwamba usomaji wake ulitabulika katika kila mkutano wa kanisa la Roma.Kama vile, wasomi wengi (Bruce na Barclay miongoni mwao) wanaamini kwamba toleo lililohaririwa la Warumi – bila marejeleo ya kibinafsi katika Warumi 16 – lilienea sana miongoni mwa makanisa ya kwanza kama muhtasari wa mafundisho ya kitume.
b. Mtumwa… mtume: Kujitambulisha kwa Paulo ni muhimu. Yeye kwanza ni mtumishi wa Yesu Kristo, na pili ameitwa kuwa mtume.
i. Kulikuwa na maneno kadhaa ya kale ya Kigiriki yaliyotumiwa mteule mtumwa, lakini wazo lililo nyuma ya neno kwa mtumishi (doulos) ni “kamilifu na utoaji kamili, si unyonge ambao ulikuwa hali ya kawaida ya mtumwa.” (Morris)
ii. Mtumishi wa Yesu Kristo, ni cheo cha juu kuliko mfalme wa ulimwengu. (Poole)
c. Kutengwa kwa injili ya Mungu: Wazo la kuwa mtume ni kwamba wewe ni balozi au mjumbe. Ujumbe wa Paulo ni injili (habari njema) ya Mungu. Ni injili ya Mungu ikimanisha ni ya mungu wa juu mbinguni. Hii si injili ambayo Paulo alitunga, yeye tu ni mjumbe wa injili ya Mungu.
i. Imetengwa kwa ajili ya injili: “Mt.Paulo Huenda hapa akarejelea hali yake ya zamani ya mfarisayo, inayo dhihirisha hali ya kutenganishwa, ama yule ametengwa. Kabla ya kutengwa kutoka kwa utumishi wa madhehebu yake mwenyewe; sasa ametengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu.” (Clarke)
ii. “Wengine wanadhani anadokeza jina la Farisayo, ambayo ni kutokana na kutengwa, alipokuwa Mfarisayo, alitengwa kwa sheria ya Mungu, na sasa akiwa Mkristo, ametengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu.” (Poole)
d. Injili ya Mungu: Barua zingine za Agano Jipya zinalenga zaidi kanisa na changamoto na matatizo yake; Warumi huzingatia zaidi Mungu. “Mungu ndiye neno muhimu zaidi katika waraka huu. Warumi ni kitabu kuhusu Mungu. Hakuna mada inayotiliwa maanani mara nyingi zaidi ya Mungu. Kila kitu ambacho Paulo anagusia katika barua hii inahusiana na Mungu. Kwa mahangaiko yetu ili kuelewa kile mtume anachosena kuhusu haki, kuhesabiwa haki, na mambo kama hayo hatupaswi kupuuza umakini wake mkuu wa Mungu.” (Morris)
i. Neno “Mungu” linapatikana mara 153 katika Warumi, wastani wa mara moja kwa kila maneno 46 – hii ni mara nyingi zaidi kuliko vitabu vingine vyote vya Agano Jipya. Kwa kulinganisha, elewa wingi wa maneno mengine yanayotumiwa katika Warumi: sheria (72), Kristo (65), dhambi (48), Bwana (43), na imani (40). Warumi inahusika na maudhui mengi tofauti lakini ni jinsi kitabu kinapaswa kuwa, ni kitabu kuhusu Mungu.
ii. Kuna maneno mengi muhimu katika msamiati wa Warumi ambayo lazima tuelewe. Bruce ananukuu utangulizi wa Tyndale kwa Warumi: “Kwanza ni lazima tuzingatie kwa makini jinsi anenavyo kwa mtume, na zaidi ya yote tujue Paulo anachomaanisha kwa maneno haya – Sheria, Dhambi, Neema, Imani, Haki, Mwili, Roho, na mengine kama hayo, kama sivyo ulisome mara kwa mara, ila utapoteza jitihada yako.”
2. (2–6) Paulo anatanguliza injili yake kwa Warumi.
Aliyoahidi Mungu hapo awali kupitia manabii wake katika Maandiko Matakatifu, kuhusu Mwanawe Yesu KristoBwana wetu, aliyezaliwa katika uzao wa Daudi kwa jinsia ya kimwili, na kutangazwa kuwa Mwana wa Mungu na ana mamlaka kulingana na Roho wa utakatifu, kwa ufufuo kutoka kwa wafu. Kwake sisi tumepokea neema na utume kwa kuitii imani miongoni mwa mataifa yote kwa ajili ya jina lake ambao ninyi pia mmekuwa miongoni mwao walioitwa kwa Yesu Kristo.
a. Aliahidi hapo awali kupitia manabii Wake: Hii injili si mpya, na sio uvumbuzi wa werevu wa mwanadamu. Ulimwengu wa Paulo ulikuwa kama wetu, ukiwa na watu waliopenda mafundisho na mafunzo “mapya”. Hata hivyo, Paulo hakuleta kitu kipya, bali kitu cha wakati wa kale katika mpango wa Mungu.
b. Kuhusu Mwanawe Yesu Kristo Bwana wetu: Hiki ndicho kitovu cha injili ya Paulo, “jua” ambalo kila kitu kingine huzunguka. Kitovu cha Ukristo si mafundisho au mfumo wa maadili, ni Mtu, Yesu Kristo.
i. Huyu Yesu ana asili ya kibinadamu (alizaliwa katika uzao wa Daudi kwa jinsi ya kimwili), na uwepo wa milele (ametangazwa kuwa Mwana wa Mungu). Ushahidi wa ubinadamu wa Yesu ni kuzaliwa kwake kama binadamu, thibitisho wa Uungu wake ni kufufuka kwake kutoka kwa wafu.
ii. Ufufuo wa Yesu unaonyesa uwezo wake wa kiungu kwa sababu alifufuka kwa uwezo wake mwenyewe: Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisa tena (Yohana 2:19).
iii. “Kuna maana kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu katika udhaifu kabla ya ufufuo, lakini Mwana wa Mungu mwenye nguvu hap baadaye.” (Morris)
c. Imetangazwa: Hili neno la kale la Kigiriki (horizo) linatokana na wazo la “kufunga, kufafanua, kuamua, au kuweka mipaka, na kwa hiyo neno letu upeo wa macho, mstari unaoamua sehemu ya mbali zaidi ya dunia inayoonekana kuambatana na mbingu. Mahali hapa neno linaashiria dhihirisho dhahiri na kamilifu la somo ili kulifanya kuwa lisilopingika.” (Clarke)
d. Yesu Kristo Bwana Wetu: inamaanisha vile Mtume Paulo alimwita Yesu Bwana: “Neno hili linalingana kama maneno ya useu. Inamaanisha kwambami wa heshima kama ‘Bwana wetu.’ Lakini pia inaweza kutumika kwa Mungu ambaye mtu anaabudu. Hata hivyo, msingi wa maana ni matumizi yake katika tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale ili kutafsiri jina la kiungu, Yahweh… Wakristo waliotumia hilo kwa Biblia yao wangefahamu neno hilo kuwa sawa na Mungu.” (Morris)
e. Kupitia kwake tumepokea neema na utume kwa ajili ya utiifu kwa imani: Injili ya Paulo iligusa maisha ya mtu kibinafsi. Si nadharia au falsafa ya kuvutia, ni habari njema zinazobadilisha maisha.
i. Injili ilimpa Paulo na kanisa neema na utume, na sababu moja ya karama hizo mbili zilitolewa ilikuwa kuzalisha utii kwa imani. “Bila NEEMA, upendeleo, na msaada wa kipekee wa Mungu, asingeweza kuwa mtume.” (Clarke)
ii. Injili ni kubwa ya kutosha na kuu kwa ulimwengu wote; lazima itoke nje ili kugusa mataifa yote.
iii. Injili ilikuwa imewafikia Wakristo wa Kirumi, kuonyesha kwamba wao ni wale walioitwa na Yesu Kristo.
3. (7–15) Nia ya Paulo kufika Roma.
Kwa wote walioko Roma, wapendwa wa Mungu, walioitwa kuwa watakatifu:
Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo.
Kwanza; Namshukuru Mungu wangu kupitia Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwamba imani yenu inazungumuzwa katika ulimwengu wote. Kwa maana Mungu ni shahidi wangu, ambaye ninamtumikia kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ili bila kukoma nawataja ninyi katika sala zangu, nikiomba ikiwa nitapata njia katika mapenzi yake Mungu kuja kwenu. Kwa maana natamani kuwaona ninyi, ili niwape karama ya rohoni, mpate kufanywa imara; ili, nipate faraja pamoja nanyi kwa imani yetu sote, yenu na yangu. Basi, wandugu, sipendi mkose kufahamu kwamba mara nyingi nilikusudia kuja kwenu (lakini nilizuiliwa hadi sasa), ili nipate matunda kati yenu pia, kama kati ya watu wa mataifa mengine. Mimi ni mdeni kwa Wagiriki na wakimataifa, kwa wenye hekima na kwa wasio na hekima. Basi, kama vile ilivyo ndani yangu, niko tayari kuihubiri Injili nanyi mlioko pia Roma.
a. Kwa wote walioko Roma: Paulo hakuwahi kufika Roma, na hakuanzisha kanisa la Kirumi. Hii inafanya Kitabu cha Warumi kuwa tofauti kwa sababu barua nyingi za Paulo zilikuwa kwa makanisa ambayo alianzisha. Inaonekana kanisa la Roma ilianza wakati Wakristo walikuja kwenye mji mkuu wa Dola na kukaa huko. Pia hakuna ushahidi wa Biblia au wa kihistoria kwamba Mtume Petro alianzisha kanisa huko Roma.
i. Matendo 2:10 inaeleza jinsi kulikuwa na watu kutoka Roma miongoni mwa Wayahudi waliokuwepo siku ya Pentekoste; waliporudi nyumbani, kulikuwa na jamii ya Wakristo huko Roma. Zaidi ya hayo, asili ya kanisa la Roma haieleweki, lakini Wakristo waliendelea kuhamia Roma kutoka sehemu zote za Dola. Haipaswi kutushangaza kwamba kanisa lilianza hapo kwa hiari, bila kupandwa moja kwa moja na mtume.
ii. Hata hivyo, kupitia kufahamiana au kupitia safari zake, Paulo aliwajua Wakristo wengi huko Roma kwa majina kwa sababu anawataja katika Warumi 16. Hata kama Paulo alijua Wakristo wengi wa Kiroma kwa kufahamiana nao, alijua mambo mawili kuwahusu na Mkristo wa kweli. Alijua walikuwa wapendwa wa Mungu na kwamba walikuwa watakatifu.
iii. Walioitwa kuwa watakatifu: “Mnaona kwamba maneno ‘kuwa’ yamewekwa na watafsiri; lakini ingawa yamehusiswa, haikuwa lazima kwa maana Waumini hawa katika Roma ‘waliitwa watakatifu.’ Hawakuitwa kwa sababu walikuwa watakatifu, bali walikuwa watakatifu kwa wito huo.” (Spurgeon)
b. Neema na iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu: Paulo anahutubia rasmi wasomaji wake kwa salamu yake ya kawaida, akiunganisha salamu ya Kigiriki ya neema na salamuya Kiyahudi ya amani. Neema hii na amani si nia njema ya mwanadamu; ni vipawa, kutoka kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo.
c. Namshukuru Mungu wangu kupitia Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwamba imani yenu itasikika ulimwengu kote. Paulo alikuwa na shukrani kwa sifa ya kanisa ya Roma na eneo iliyomo, kanisa hili lilikuwa na mwonekano maalum na fursa ya kumtukuza Yesu katika himaya yote.
i. Wakristo hawa walipaswa kuwa na nguvu; Wakristo wa Roma hawakupendwa na watu wengi – waliaminika kuwa ‘maadui wa binadamu’ na walitajwa kuwa na tabia mbaya kama vile ndoa kati ya jamii na kula nyama za watu. Kwa idadi kubwa, basi, wakawa wahasiriwa wa unyanyasaji wa kifalme – na ni mateso haya ya Wakristo chini ya Nero ambayo hujenga msingi wa mauaji wa Paulo. (Bruce)
ii. “Warumi wanahimiza mahali hapa kuthibitisha Roma kuwa kanisa anzilishi au kanisa kuu lakini bila sababu, kanisa la Thesalonike lilikuwa na sifa ya juu sana, angali 1 Wathesalonike 1:8.” (Poole)
d. Bila kukoma nawataja sikuzote katika maombi yangu: Paulo alitaka Wakristo wa Kiroma wajue kwamba alikuwa anawaombea na kuombea nafasi ya kuwatembelea (nipate njia katika mapenzi ya Mungu kuja kwenu).
i. “Sio ajabu kwamba walifanikiwa vyema sana kila mara Paulo alipowataja katika sala zake. Baadhi ya makanisa yangefanikiwa zaidi ikiwa baadhi yenu mngewakumbuka katika maombi.” (Spurgeon)
ii. Kwa maana Mungu ni shahidi wangu labda ni hakikisho wa Paulo jinsi ilivyo rahisi kusema utamwombea mtu fulani, halafu ukashidwa kufanya hivyo. Alitaka wajue hakika kwamba kweli aliwaombea.
e. Naweza kutoa… ili nitiwe moyo: Nia ya Paulo kutembelea kanisa la Roma haikuwa tu kutoa, bali kupokea pia, kwa sababu Paulo alitambua kwamba katika imani yao walikuwa na kitu cha kutoa.
f. Mara nyingi nilipanga kuja kwenu (lakini nilizuiliwa hadi sasa): Kwa muda mrefu Paulo alitaka kwenda Roma na alizuiliwa tu na mazingira ya nje. Labda baadhi ya maadui wa Paulo walidokeza kwamba aliogopa kwenda Roma na kuhubiri injili katika “makundi makuu,” katika jiji kuu la Himaya.
g. Mimi ni mdeni kwa Wagiriki na wasio Wayahudi, kwa wenye hekima na pia wasio na hekima: Paulo alitambua kwamba alikuwa na deni kwa Roma. Milki ya Kiroma ilileta amani na utulivu kwa ulimwengu; walileta utamaduni, na mfumo bora wa usafiri kwa ulimwengu. Paulo alitumia haya yote kueneza Injili; angelipa vizuri deni hili kwa kuipa Roma habari njema ya Yesu Kristo.
i. Paulo alikuwa mwinjilisti asiyechoka, alifanya kazi duniani kote kwa sababu aliamini alikuwa na deni la kulipa, na ilikuwa deni ya ulimwengu mzima.
h. Niko tayari: Spurgeon alijiuliza ikiwa Paulo hakutumia neno “niko tayari”kama kauli mbiu yake. Kama maneno ya kwanza kutoka kinywani mwake alipookoka yalikuwa, “Bwana, wataka nifanye nini?” (Matendo 9:6).
∙ Paulo alikuwa tayari kuhubiri na kutumika (Warumi 1:15).
∙ Paulo alikuwa tayari kuteseka (Matendo 21:13).
∙ Paulo alikuwa tayari kufanya kazi isiyopendeza (2. Wakorintho 10:6).
∙ Paulo alikuwa tayari kufa (2 Timotheo 4:6).
i. “Mmoravian alikuwa karibu kutumwa na Zinzendorf kuhubiri Greenland. Hakuwahi kuisikia; lakini kiongozi wake alimwita, na kusema, ‘Ndugu, utaenda Greenland?’ Akajibu, Ndiyo, bwana. ‘Utaenda lini?’ ‘Wakati buti langu litaletwa nyumbani kutoka kwa fundi wa viatu;’ na alienda mara tu buti zake zilifika nyumbani. Hakutaka kitu kingine ila jozi hiyo tu la buti, na alikawa tayari kwenda. Paulo, bila hata kungoja buti zake ziletwei nyumbani kutoka kwa mtu wa kushona viatu, anasema, ‘Niko tayari.’ Lo, ni jambo la kustaajabisha kupata mtu amenaswa kiasi kwamba anaweza kwenda mahali ambapo Mungu angemtaka aende, na anaweza kwenda mara moja.” (Spurgeon)
i. Niko tayari kuwahubiria ninyi mlioko Roma pia: Huu ni ujasiri wa kunena. “ongea juu ya watu wako wajasiri, watu wakuu, Ee ulimwengu! Ni wapi katika historia yote unaweza kupata mtu kama Paulo? Alexander, Kaisari, Napoleon, waliandamana na ulinzi wa majeshi yao ili kutekeleza matakwa yao juu ya wanadamu. Paulo alikuwa tayari kutembea na Kristo peke yake hadi katikati ya ukuu wa ulimwengu huu uliokita mizizi chini ya Shetani kwa neno la msalaba, ambalo yeye mwenyewe anasema ni kosa kwa Wayahudi; na watu wa mataifa mengine upumbavu.” (Newelli)
i. Ajabu – katika siri ya Mungu isiyo eleweka kwa urahisi- Paulo hatimaye alipofika Roma, alikuja kama mfungwa.
ii. “Sidhani kama Paulo aliwahi fikiri kwamba angetumwa huko kwa gharama ya serikali, lakini alikuwa. Milki ya Kiroma ililazimika kumtafutia meli,maaskari shupavu wa kumsindikiza pia,na akaingia mjini kama balozi akiwa mfungwa. Mioyo yetu inapotamania jambo, na tuliombee, Mungu anaweza kutupa baraka hiyo lakini, inaweza kuwa, kwa namna ambayo hatukuitarajia kamwe. Utaenda Roma, Paulo; lakini utaenda kwa minyororo.” (Spurgeon)
4. (16–17) Paulo anatanguliza kiini cha barua yake: haki ya Mungu, kama inavyofunuliwa katika Injili ya Yesu Kristo.
Kwa maana sioni haya kwa Injili ya Yesu Kristo, kwa maana ni uwezo wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, Kwanza kwa Myahudi na pia Myunani. Maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, “Mwenye haki ataishi kwa imani.”
a. Baada ya utangulizi wake, Paulo anatanguliza kauli yake “nadharia” Waraka wake kwa Warumi. Leon Morris asema hivi kuhusu Warumi 1:16 na 17: “Mistari hii miwili ina umuhimu kupita kiasi cha urefu wake.”
b. Sioni haya injili: Hii inadhihirisha moyo wa Paulo. Katika jiji ya hali ya juu ya Roma, wengine wanaweza kuaibishwa na injili inayozingatia Mwokozi wa Kiyahudi aliyesulubiwa na angekumbatiwa na watu wa tabaka la chini kabisa – lakini Paulo haoni haya.
c. Kwa maana ni uwezo wa Mungu uuletao wokovu kwa kila aaminiye: Ndiyo maana Paulo haoni haya juu ya injili inayohusu Mwokozi aliyesulubiwa. Anajua kwamba injili – habari njema ya Yesu Kristo – ina uwezo asili. Hatuipei uwezo, tunazuia uwezo wa injili tunapoiwasilisha kikamilifu.
i. Injili hakika ni habari, lakini ni zaidi ya habari; ina nguvu ya asili. “Injili sio ushauri kwa watu, ikipendekeza kwamba wajiinue. Ni uwezo, Inawainua juu. Paulo hasemi kwamba injili huleta nguvu, bali kwamba ni uwezo, na uweza wa Mungu.” (Morris)
ii. Haswa, jiji la Roma lilifikiri kwamba ilijua yote kuhusu mamlaka: “Mamlaka ndicho kitu ambacho Roma ilijivunia zaidi. Ugiriki inaweza kuwa na falsafa yake, lakini Roma ilikuwa na mamlaka yake” (Wiersbe). Licha ya uwezo wao wote, Warumi – kama watu wengine – hawakuwa na uwezo wa kujifanya waadilifu mbele za Mungu. Mwanafalsafa wa kale Seneca alitaja Roma “dimbwi la uovu” na mwandishi wa kale Juvenali aliliita “mfereji wa maji machafu ambamo sira za ufalme huo hufurika.”
iii. Kwa wokovu: Katika ulimwengu wa Warumi wa siku za Paulo, watu walitazamia wokovu. Wanafalsafa walijua mwanadamu alikuwa mgonjwa na alihitaji msaada. Epiktetusi aliita chumba chake cha mihadhara “hospitali ya mioyo iliyogonjeka.” Epikurusi aliliitaja fundisho lake “dawa ya wokovu.” Seneka alisema hivyo kwa sababu wanadamu walitambua sana “udhaifu wao na kutofaulu kwao katika mambo ya lazima” hivi kwamba watu wote walikuwa wakitazamia “wokovu.” Epiktetusi alisema watu walikuwa wakitafuta amani “si ya tangazo la Kaisaria, bali la Mungu.” (Imetajwa katika Barclay)
iv. Uwezo wa Injili uletao wokovu huja kwa kila aaminiye. Mungu hatamnyima wokovu yeye aaminiye; bali kuamini pekeendiko kunahitajika.
d. Kwanza kwa Myahudi na pia Mgiriki: Huu ni mfano wa uenezaji wa injili, unaoonyeshwa na huduma ya Yesu (Mathayo 15:24) na huduma ya kwanza ya wanafunzi wa Yesu (Mathayo 10:5–6).
i. Hii ina maana kuwa injili ilikusudiwa kwenda mwanzo kwa Wayahudi wa mila na kitamaduni, na kisha kwa Wagiriki wa kitamaduni. “Wakati huu neno Kigiriki lilikuwa limepoteza maana yake ya ubaguzi wa rangi kabisa. Haikumaanisha mzaliwa wa nchi ya Ugiriki… [Mgiriki] alikuwa ni mtu anayejua utamaduni na mawazo ya Ugiriki.” (Barclay)
e. Kwa maana ndani yake haki ya Mungu inadhihirishwa: Kwa urahisi, injili inadhihirisha haki ya Mungu. Ufunuo huu wa haki ya Mungu huja kwa wale walio na imani, kutimiza Habakuki 2:4: Wenye haki – yaani, wale waliohesabiwa haki – wataishi kwa imani.
i. Ni muhimu kuelewa hasa maana ya haki ya Mungu iliyofunuliwa na injili. Haisemi juu ya haki takatifu ya Mungu inayomhukumu mwenye dhambi, bali juu ya aina ya haki ya Munguambayo hutolewa kwa mwenye dhambi anayeweka tumaini lake kwa Yesu Kristo.
ii. Uadilifu: William Barclay anafafanua maana ya neno hili la kale ya Kiyunani dikaioo, linalomaanisha ninalithibitisha, na ni mzizi wa dikaioun (haki): “Vitenzi vyote katika Kigiriki vinavyoishia kwa oo… daima humaanisha kuwajibika, au kutambulika au kumkumbuka mtu kama kitu. Mungu akimhesabia haki mwenye dhambi, haimaanishi kwamba anapata sababu za kuthibitisha kuwa alikuwa mwema – mbali nayo, hata haimaanishi kwamba wakati huu anamfanya mwenye dhambi kuwa mtu mwema.Bali ina maana kwamba Mungu humchukua mwenye dhambi kama hakuwa mwenye dhambi hata kidogo.”
iii. “Ilikuwa siku ya furaha katika maisha ya Luther alipogundua kwamba ‘Haki ya Mungu’ kama inavyotumika katika Warumi inamaanisha hukumu ya Mungu ya haki juu ya mwumini.” (Lenski)
iv. Tamko hili ni la maana zaidi tunapoelewa hii ni haki ya Mungu inayotolewa kwa mwumini. Si haki ya yule mtu mtakatifu zaidi, wala si haki ya Adamu asiye na hatia katika Edeni. Ni haki ya Mungu. “Uadilifu unaoleta kuhesabiwa haki ni ule unaodhihirishwa na ukamilifu wa yote ambayo Mungu analo na anafanya, Ni ‘haki ya Mungu’.” (Murray)
v. Imani hii (tumaini) katika Yesu Kristo inakuwa msingi wa maisha kwa wale wanaohesabiwa haki (kutangazwa kuwa wenye haki); kweli, wenye hakiwataishi kwa imani. Hawaokolewi kwa imani tu, bali wanaishi kwa imani.
f. Kutoka imani hadi imani: Wazo ya kifungu hiki kigumu pengine ni kwa imani tangu mwanzo hadi mwisho. Biblia ya NIV inatafsiri kifungu kutoka imani hadi imani kama kwa imani kutoka kwanza hadi mwisho.
i. “Hasemi, toka imani hata matendo, wala kutoka matendo hata imani; bali toka imani hadi imani, yaani kwa imani tu.” (Poole)
ii. “Pengine inachoeleza ni ukumbusho kwa mwamini kuhalalisha imani ni mwanzo tu wa maisha ya Mkristo. Mtazamo huo huo lazima umtawale katika uzoefu wake wa kuendelea kama mwana wa Mungu.” (Harrison) Huu ni kielelezo cha ujumbe wa Paulo katika Wagalatia 3:1–3.
C. Kwa nini mwanadamu lazima ahesabiwe haki kwa imani: hatia ya jamii ya wanadamu kwa ujumla.
1. (18a) Hatari kuu inayowakabili wanadamu: ghadhabu ya Mungu.
Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni
a. Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni: Wazo hili ni sahihi lakini linatisha– ghadhabu ya Mungu inadhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya wanadamu, na wanadamu wanastahili ghadhabu ya Mungu.
b. Ghadhabu ya Mungu: Wakati mwingine tunapinga wazo la ghadhabu ya Mungu kwa sababu tunailinganisha na hasira ya kibinadamu, ambayo inachochewa na sababu za kibinafsi au na hamu ya kulipiza kisasi. Hatupaswi kusahau kwamba ghadhabu ya Mungu ni ya haki kabisa katika tabia.
i. Si lazima, na inadhoofisha dhana ya kibiblia juu ya ghadhabu ya Mungu, kuinyima tabia yake ya kihemko na ya kugusa … kutafsiri ghadhabu ya Mungu kama kusudi lake la kuadhibu dhambi au kupata uhusiano kati ya dhambi na taabu. ni kusawazisha ghadhabu na athari zake na kuondoa ghadhabu kama harakati ndani ya akili ya Mungu. Ghadhabu ni chukizo takatifu la nafsi ya Mungu dhidi ya kile ambacho ni ukinzani wa utakatifu wake.” (Murrary)
ii. Katika Warumi 1:16, Paulo alizungumza juu ya wokovu – tunaokolewa kutokakwa nini? Kwanza kabisa, tunaokolewa kutoka kwa ghadhabu ya Mungu ambayo kwa haki tunastahili. “Pasipo kitu cha kuokolewa kutoka, hakuna maana katika kuzungumza juu ya wokovu.” (Morris)
c. Ghadhabu ya Mungu: Katika sehemu hii ya barua (Warumi 1:18–3:20), lengo la Paulo si kutangaza habari njema, bali ni kuonyesha uhitaji kamilifu wa habari njema ya wokovu kutoka kwa ghadhabu ya Mungu iliyo ya haki
i. Ghadhabu ya Mungu haijafunuliwa katika injili, lakini katika ukweli wa uzoefu wa mwanadamu.
2. (18b–23) Sababu ya wanadamu kuwa na hatia mbele za Mungu, nidhihirisho ya uasi na uovu ya wanadamu.
Juu ya uasi na uovu wote wa wanadamu, waipingao ukweli kwa udhalimu; kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana ni dhahiri ndani mwao, maana Mungu amewaonyesha. Tangu kuumbwa kwa ulimwengu sifa zake sisizoonekana tangu kuumbwa ulimwengu zinaonekana, na kufahamika kwa kazi zake, yaani, uwezo wake wa milele na Uungu wake, hata wasiwe na udhuru, kwa maana, ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza kama Mungu, wala hawakumshukuru, bali walifanya ubatili katika fikira zao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinenea kuwa wenye hekima walipumbazika, wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya mwanadamu aliye na uharibifu, na ndege na wanyama wenye miguu minne na vitambaavyo.
a. Kutomcha Mungu: Hii inarejelea makosa ya mwanadamu dhidi ya Mungu. Udhalimu unamaanisha dhambi za mwanadamu dhidi ya mwanadamu.
b. Wanaokandamiza ukweli kwa udhalimu: Wanadamu kwa kweli wanaikandamiza kweli ya Mungu. Kila ukweli uliofichuliwa kwa mwanadamu na Mungu umepigwa vita, kupuuzwa, na kufichwa kwa makusudi.
c. Sifa zake zisizoonekana zinaonekana wazi: Mungu anatuonyesha mambo fulani kwa uwezo wake wa milele na asili ya kimungu kupitia uumbaji, kwa vitu vilivyofanywa. Ametoa ufunuo wa jumla ulio dhahiri katika uumbaji na ndani ya akili na mioyo ya mwanadamu.
i. Inavyoonekana wazi: Tabia ya kiulimwengu ya ufufunuo huu na ubainifu wake humwacha mwanadamu bila kizingizio cha kuikataa. “Wanadamu hawawezi kumshtaki Mwenyezi Mungu kwa kujificha kwao na hivyo kutoa udhuru kwa uasi na uasherati wao.” (Lenski)
d. Ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza kama Mungu: Tatizo sio kwamba mwanadamu hakumjua Mungu, lakini kwamba alimjua – lakini alikataa kumtukuza kama Mungu. Kwa hiyo, mwanadamu hana udhuru. Badala ya kumtukuza Mungu tuligeuza wazo letu kwake kuwa maumbo na taswira nzuri zaidi zakupendeza mioyo yetu mbovu na iliyotiwa giza.
i. “Je, utatambua, kulingana na andiko langu, ujuzi sio kitu ikiwa hauelekezi kwenye mazoezi matakatifu? ‘Walimjua Mungu.’ lakini halikuwafaidi, kwa maana ‘hawakumtukuza kama Mungu.’ Kwa hiyo rafiki yangu wa kitheolojia, ambaye anajua mengi sana kwamba anaweza kupasua nywele juu ya mafundisho, haijalishi unafikiri nini, au unajua nini, isipokuwa inakuongoza kumtukuza Mungu, na kuwa na shukrani.” (Spurgeon)
ii. Hatuwezi kuonekana kupinga jaribu la kumuumba Mungu kwa sura zetu potovu, au hata kwa sanamu iliyo chini yetu. Cha kusikitisha tunakuwa kama Mungu tunayemtumikia.
iii. Ni muhimu kwamba mara kwa mara tulinganishe dhana yetu wenyewe dhidi ya uhalisia wa Mungu, kama unavyofunuliwa katika neno Lake. Tunaweza pia kuwa na hatia ya kumwabudu Mungu tuliyemuumba.
iv. Taswira katika Warumi 1:23 ni neno la kale la Kiyunani eikon. Ni jambo la hatari kubadili utukufu wa Mungu asiyeharibika kuwa eikon (sura) wa chaguo lako mwenyewe.
e. Bila shukran: Kutokuwa na shukrani kwa mwanadamu dhidi ya Mungu ni jambo la kushangaza. “Siwezi kusema chochote kibaya zaidi kuhusu binadamu kwamba hana shukrani kwa wale ambao wamekuwa wafadhili wake, na unaposema hana shukurani kwa Mungu, umesema juu ya jambo baya zaidi uwezalo juu yake.” (Spurgeon)
i. Lakini unapomtukuza Mungu kama Mungu, na kushukuru kwa kila kitu – wakati unachukua mkate na kikombe cha maji baridi, na kusema na Puritan maskini, ‘Je, haya yote, na Kristo pia?’ – ndipo unapata furaha, na kufurahisha wengine. Mhubiri mcha Mungu, alipogundua kwamba chakula cha jioni kilikuwa viazi na tunguli, alimshukuru Mungu kwamba alikuwa amepora bahari na nchi kavu ili apate chakula cha watoto wake. Roho wa shukran kama huu huzaa upendo kwa kila mtu, na humfanya mtu kuupitia ulimwengu kwa uchangamfu.” (Spurgeon)
f. Wakijidai kuwa wenye hekima, wakawa wapumbavu: Kukataa kwetu kwa ufunuo wa Mungu hakutufanyi sisi kuwa shupavu au bora zaidi. Badala yake, inawafanya wanadamu kuwa wabatili katika mawazo yao, na kuifanya mioyo yetu ya kipumbavu kuwa giza – nasi tunakuwa wapumbavu.
i. Ukweli ni kwamba mtu akishakataa ukweli ya Mungu iliyo ndani ya Yesu, ataangukia kila jambo potovu, na kuamini mifumo dhaifu na la wazo potovu zaidi kuliko ile anayokataa kutoka kwa Mungu.
ii. Ubatili huu wa fikira, kutiwa giza kwa moyo, na upumbavu lazima uonekane kama mfano mmoja wa ghadhabu ya haki ya Mungu dhidi ya wale wanaokataa kile anachofunua. Moja ya hukumu yake dhidi yetu ni kuturuhusu kupata matokeo mabaya yanayoletwa na mwenendo wetu wa dhambi.
3. (24–32) Matokeo mabaya ya hatia ya mwanadamu mbele za Mungu.
Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha, katika tamaa za mioyo yao, hata wakavunjiana heshima miili yao,kwa maana waliibadili ukweli wa Mungu kuwa uongo, wakakishujudia kiumbe na kukiabudu badala ya muumba anayehimidiwa milele Amina. Kwa sababu ya hayo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao mbaya. Hata wanawake wao walibadilisha matumizi ya asili kwa yasiyo asili. Vivyo hivyo wanaume nao waliacha matumizi ya asili ya mwanamke, wakawakiana tamaa, wanaume wakitenda yasiyopaswa kufanya nafsini mwao,kwa malipo ya upotevu wao waliyostahili. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa, wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu, tamaa, ubaya, kujaa husuda, uuaji, fitina, hadaa,watu wa nia mbaya; ni wachongezi, wasengenyaji, wenye kumchukia Mungu, wajeuri, wenye kiburi, wenye majivuno,wenye kutunga mabaya, wasiotii wazazi wao, wasio na fahamu, wasioaminika, wasio na upendo, wasiosamehe, wasio na rehema; wakiijua hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wanastahili mauti, wazitenda na si hivyo tu, bali wanakubaliana na wayatendao.
a. Kwa hiyo Mungu pia aliwaacha: Katika ghadhabu yake ya haki na hukumu, Mungu humwachilia mwanadamu kwenye dhambi ambayo mioyo yetu inatamani, na kuturuhusu kupata matokeo ya dhambi. Maneno haya ni muhimu sana Paulo anayarudia mara tatu katika kifungu hiki.
i. Hosea 4:17 inaeleza kipengele cha hukumu ya Mungu “anayetutoa,” akituacha kwenye dhambi zetu wenyewe: Efraimu amejiungamanisha na sanamu, mwache.
ii. Tunafanya makosa tunapofikiri kwamba ni rehema au fadhili za Mungu zinazomruhusu mwanadamu kuendelea katika dhambi. Kwa hakika ni ghadhabu yake inayoturuhusu kuendelea kujiangamiza wenyewe kwa dhambi.
b. Walioubadili ukweli wa Mungu kuwa uwongo: Katika kila uasi na kutotii dhidi ya Mungu tunaubadili ukweli wa Mungu kwa uongo tuliouchagua sisi wenyewe, na kukiweka kiumbe mbele ya Muumba.
i. Paulo anatumia kifungu mahusuzi – sio udanganyifu, bali ni uongo. Uongo huo ni ibada ya sanamu – ambayo hutuweka pahali pa Mungu. Ni uongo utakuwa kama Mungu (Mwanzo 3:5).
c. Kwa sababu hii Mungu aliwaacha wafuate tamaa yao: Paulo aliandika haya akiwa katika jiji la Korintho, ambamo kila aina ya uasherati na ukahaba wa kitamaduni ulifanywa kwa huru. Desturi ya Warumi 1:24 inahusu mchanganyiko huu wa usherati na ibada ya sanamu.
i. Hili ni chanzo cha kifungu ambapo Paulo anaelezea dhambi na upotovu wa kipagani kwa uwazi – Kwa uwazi kwamba Spurgeon alifikiri kifungu hiki hakifai kwa usomaji wa umma. “Sura hii ya kwanza ya Waraka kwa Warumi ni sehemu ya kuogofya ya neno la Mungu. Nisingependa kuisoma kwa sauti; haikusudiwa kutumika hivyo. Isome nyumbani, na ushangazwe na maovu mabaya ya ulimwengu wa Mataifa.” (Spurgeon)
d. Hata wanawake wao walibadili matumizi ya asili: Paulo anamanisha ushoga – kati ya kike na waume – kama kielelezo cha Mungu akiwaachalia wanadamu kwenye uchafu na tamaa.
i. Wengine husema hakuna mahali Biblia inashutumu ushoga, lakini katika Warumi 1:27 inaweka wazi dhambi ya ushoga inayolaaniwa katika Warumi 1:27 inahusishwa na dhambi ya wanawake iliyotajwa katika Warumi 1:26.
ii. Paulo hata hatumii maneno ya kawaida kwa wanaume na wanawake hapa; anatumia maneno ya kiume na kike, akitumia kategoria zinazoelezea kujamiiana nje ya kibinadamu, kwa sababu aina ya dhambi ya zinaa anayoielezea ni nje ya utu wa mwanadamu.
iii. Paulo anaainisha sehemu nzima kama wazo la tamaa mbaya – zisizo na afya, zisizo takatifu. Hata hivyo, Paulo aliishi katika tamaduni ambao ulikubali ushoga. Paulo hakuandika haya kwa utamaduni uliokubaliana naye.
iv. Paulo aliandikia tamaduni ambapo ushoga ulikubaliwa kama sehemu ya maisha kwa wanaume na wake. Kwa miaka 200 hivi, wanaume waliotawala Milki ya Roma walifanya gono mara nyingi na wavulana wachanga waziwazi.
v. Wakati fulani, Milki ya Roma ilitoza ushuru ukahaba ulioidhinishwa wa ushoga na kuwapa makahaba wa kiume likizo ya halali. Ndoa ya kisheria kati ya wanandoa wa jinsia moja ilitambuliwa, na hata baadhi ya wafalme walioa wanaume. Wakati huu Paulo akiandika, Nero alikuwa mfalme. Alichukua mvulana aitwaye Sporasi na akahasiwa, kisha akamwoa (kwa sherehe kamili), akamleta kwenye jumba la kifalme kwa maandamano makubwa, na kumfanya mvulana huyo kuwa mke wake. Baadaye, Nero aliishi na mwanamume mwingine, na Nero alikuwa “mke.”
vi. Katika tamaduni za kisasa, mazoea ya ushoga yanaonyesha kuwaacha kwenye uchafu, katika tamaa za mioyo yao, ili kuvunja heshima miili yao kati yao wenyewe. Utafiti wa 2013 ulionyesha wanaume wanaoshiriki gono na watu wa jinsia moja wana uzoefu wa ngono sio kwa mara ya kwanza, wana wenzi wengi katika maisha yao yote, na wana uwezekano mkubwa wa kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja ikilinganishwa na uhusiano wa jinisia tofauti kati ya wanaume na au wanawake. Mashoga wa kiume pia walikuwa na wapenzi wengi waliokuwa wakubwa au wadogo kiumri, ikilinganishwa na uhusiano wa jinsia tofauti ya wanaume na wanawake. (Glick, Morris, Foxman; https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3334840/)
vii. Utafiti mwingine unaonyesha wapenzi wa jinsia moja ya wanaume wana wapenzi wengi (4 au zaidi katika miezi 12 iliyopita) mara tatu ya kiwango cha wanaume walio na wapenzi wa jinsia tofauti na karibu mara nane kiwango cha wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsia tofauti. (Uingereza, Brown, https://contexts.org/blog/an-unequal-distribution-of-partners-gays-versus-straights/)
e. Wakipokea adhabu ya kosa lao iliyostahili: Paulo anazungumza juu ya adhabu ya tendo la mashoga; ushoga una adhabu ndani yake. Hii inazungumzia juu ya asili ya dhambi ya kujiangamiza kwa ujumla; mara nyingi hubeba ndani mwake adhabu yake yenyewe.
i. Wakati mwingine ni adhabu ya ugonjwa, ambayo ni matokeo ya kukiuka utaratibu wa desturi. Wakati mwingine ni adhabu ya uasi, na kusababisha upweke wa kiroho na matokeo yake. Kwa maana hii neno ‘shoga’ ni matamanio. Inatuma ujumbe kuna kitu cha kufurahisha na kisichojali kuhusu maisha ya ushoga – ambayo haipo.
f. Tena, “uhuru” wa kutotii unapaswa kuonekana kama hukumu ya Mungu, siyo wema wake; wanaojihusisha na vitendo hivyo wanajipatia nafsini mwao adhabu ya makosa yao.
g. Kwa hukumu zaidi, Mungu humkabidhi mwanadamu kwa kudhalalisha, ili mambo ya aibu na ya kuumiza yakubaliwe na kuidhinishwa.
i. Neno kudhalilishwa (au, kukataliwa katika KJV) lilimaanisha “kile ambacho hakijastahimili jaribio.” Ilitumiwa kwa sarafu ambazo zilikuwa chini na hivyo kukataliwa. Wazo ni kwamba mwanadamu “hakubali” kumjua Mungu, walikuwa na akili “isiyokubalika.”
ii. “Wanadamu walimjaribu Mungu kwa kusudi la kumwidhinisha iwapo atatimiza masharti yaliyomweka kama Mungu ambaye angempendeza, na kupata kwamba hakutimiza masharti hayo, walikataa kumwidhinisha kuwa yeye ni Mungu. Mungu anayepaswa kuabudiwa, au awe n katika ujuzi wake.” (Wuest)
iii. Akili iliyoharibika: Uasi wetu dhidi ya Mungu hauonyeshwi tu katika matendo yetu, bali katika kufikiri kwetu. Sisi ni “wazimu kiroho” katika uasi wetu dhidi ya Mungu.
h. Orodha katika Warumi 1:29–31 inatoa mifano hasaa ya aina ya mambo hayafai. Angalia jinsi dhambi “hazikubaliki katika jamii” (kama vile kutamani, husuda na kiburi) zinajumuishwa kama dhambi “zisizokubalika katika jamii” (kama vile kuua na kutokuwa na upendo).
i. Tamaa: Neno hili huelezea mwazo wa kuwa na zaidi.
ii. Wanong’ona: “Watusi wa siri; wale, chini ya usiri hujifanya, hubeba shutuma dhidi ya jirani zao, ziwe za kweli au uongo; wakiharibu sifa zao kwa maneno ya siri.” (Clarke)
iii. Wivu: Je, hii ni dhambi ndogo? Wivu ina nguvu sana ndiyo ilimweka Yesu msalabani. Pilato alijua wamemkabidhi kwa sababu ya wivu (Mathayo 27:18).
iv. Wenye kiburi:“Wale wanaojiinua nafsi zao kila wakati na kuwashusha wengine; wakijitukuza kwa gharama ya jirani zao; na wakitaka watu wote wayapokee maneno yao kama usia. (Clarke)
i. Wale wanaotenda au kukubali mambo haya wanastahili kifo; ndio walengwa wanaostahili ghadhabu ya Mungu.
j. Jeuri, uasherati, ukatili na udhalilishaji unatoka wapi? Inatokea wakati wanadamu wanaacha maarifa ya kweli ya Mungu, na hali ya jamii inaakisi hukumu ya Mungu juu yao kwa haya.
© 2024 The Enduring Word Bible Commentary by David Guzik – [email protected]